Header Ads

AL AHLY YAIPIKU AC MILAN KWA KUNYAKUA MATAJI MENGI DUNIANI

WANAHABARI WAITAKA MILAN KUBADILI JEZI ZAO ZILIZOANDIKWA: “IL CLUB PIU TITOLATO AL MONDO”!!!
AL_AHLY_LOGOCAF imetangaza kuwa Vigogo wa Egypt, Al Ahly, ambao Wikiendi hii wataivaaAC_MILAN-NEMBO_BORA_DUNIANI Yanga kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI, wamewapiku Vigogo wa Italy, AC Milan, kwa kuwa na Mataji mengi ya Kimataifa Duniani.
Baada CAF kutoboa mafanikio ya Al Ahly, huko Italy Wanahabari wameitaka AC Milan kuondoa Lebo ya Jezi zao inayosomeka: “Il Club Piu Titolato Al Mondo” ikimaanisha “Klabu yenye Mafanikio Makubwa Duniani” kwa vile Al Ahly sasa wana Mataji ya Kimataifa 19 ukilinganisha na 18 ya AC Milan.
Wiki iliyopita, Al Ahly walinyakua Taji lao la 19 baada ya kuichapa Klabu ya Tunisia CS Sfaxien Bao 3-2 na kubeba CAF SUPER CUP.
Makamu Rais wa AC Milan, Adriano Galliani, amesema wataomba msaada wa FIFA ili kuthibitisha Mataji ya Al Ahly kabla hawajabadili Jezi zao kama Wanahabari walivyoshauri.
Nae Rais wa CAF, Issa Hayatou, amewapongeza Al Ahly: “Hongera kwa Al Ahly kwa mafanikio haya ya Kihistoria! CAF inasikia fahari kwa kuiweka Afrika kwenye Ramani ya Dunia kwa mara nyingine. Hili ni jambo bora kwa Soka la Afrika na linathibitisha hatua kubwa zilizofikiwa na hii itahamasisha Klabu nyingine kufanya zaidi.”
MATAJI
AL AHLY-19:
-CAF Champions League 8 [1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012, 2013]
-CAF Cup Winners’ Cup 4 [1984, 1985, 1986, 1993]
-CAF Super Cup 6 [2002, 2006, 2007, 2009, 2013, 2014]
-Afro-Asian Cup 1 [1988]
AC MILAN-18:
-UEFA Champions League 7
-UEFA Super Cup 5
-UEFA Cup Winners’ Cup 2
-Intercontinental Cup 3
-FIFA Club World 1.

Powered by Blogger.