Header Ads

UCL: MAFANIKIO MAN UNITED MIKONONI MWA ROONEY & ROBIN VAN PERSIE!

MOYES: ‘WAWILI HAO NI MUHIMU KWA KILA KITU CHETU!!’
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
+++++++++++++++++++++++++++++++++
RVP_N_ROONEYWAKATI Mabingwa wa England, Manchester United, Usiku huu watatinga ndani ya Karaiskakis Stadium, Jijini Athens, Ugiriki  kucheza na Olympiakos kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Meneja wao, David Moyes, amesema mafanikio yao yapo mabegani mwa Mastaa wao wawili, Wayne Rooney na Robin van Persie.
Msimu uliopita, Rooney na Van Persie walijenga ushirikiano mzuri na kuisaidia Man United kutwaa Ubingwa na mapema Msimu huu walianza vyema na wote haraka kupiga Bao nyingi lakini kuanzia mwanzoni mwa Desemba walikuwa nje kwa kipindi kirefu wakiwa majeruhi na wameanza kucheza tena pamoja Mechi 5 tu zilizopita.
Akiongea kabla ya Mechi ya Leo, David Moyes amesema: “Wao ni muhimu kwa vitu vingi tunavyofanya. Ni Wachezaji wazuri sana. Rekodi yetu tukiwa nao ni nzuri sana kupita tukiwakosa.”
Nae Rooney alisema hatakuwa na furaha hadi atwae UCL kwa mara ya pili na pia alimsifia Mshirika wake Robin van Persie kwa kutamka: “Robin ni Mchezaji hodari sana, na ni mmoja wa Wafungaji wazuri mno Duniani. Kama Meneja alivyosema tuna rekodi nzuri tukicheza pamoja. Lakini bahati mbaya tuliumia kwa wakati mmoja Msimu huu.”
Msimu huu, Rooney na Van Persie wamefunga Jumla ya Bao 26 katika Mechi 50 na ni 3 za kwenye UCL huku Rooney akiwa na 2 na Van Persie 1.
Man United na Olympiakos zimeshakutana mara 4 kwenye UCL, kwenye Makundi Misimu ya
2001/02 na 2002/03 na Man United kushinda Mechi zote 4.
VIKOSI VINAWEZA KUWA:
OLYMPIAKOS: Roberto, Holebas, Papadopoulos, Leandro, Salino, Manolas, Machado, Ibagaza, Samaris, Campbell, Perez.
MANCHESTER UNITED: De Gea, Evra, Vidic, R Ferdinand, Smalling, Januzaj, Carrick, Fletcher, Valencia, van Persie, Rooney
REFA: Gianluca Rocchi [Italy]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MATOKEO:
Jumanne Februari 18
Manchester City 0 FC Barcelona 2
Bayer 04 Leverkusen 0 Paris Saint-Germain 4
Jumatano Februari 19
AC Milan 0 Atletico de Madrid 1
Arsenal FC 0 Bayern Munich 2
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP
Powered by Blogger.