Matumizi Ya Kiswahili ZINDUKA yataka kitumike kwenye mijadala Afrika Mashariki
Jumuiko la makundi mbalimbali ya
kijamii kutoka nchi za Afrika Mashariki kupitia umoja wao unaojulikana kama
“ZINDUKA”,limekuja na mapendekezo ya kutaka matumizi rasmi ya lugha ya
Kiswahili, katika mijadala na mikutano yote ya jumuiya ya Afrika mashariki.
Katika uwasilishwaji wa
mapendekezo kutoka katika kusanyiko hilo la “ZINDUKA” lililokuwa likifanyika
Jijini Arusha, ni kwamba Kiswahili hakijapewa uzito unaostahili ndani ya Afrika
Mashariki.
Mmoja wa wasilishaji wa
mapendekezo hayo Hezekiel Gikambi mhariri wa jarida la Swahilihub kutoka Kenya
amesema katika jumuiya zote za afrika na hata ulaya hakuna hata moja miongoni
mwazo ambayo ina lugha moja lakini Afrika mashariki ina Kishwahili ambacho hata
hivyo hakitumiki ipasavyo
Masuala mengine yaliyozungumzwa
katika kusanyiko hilo ni pamoja na kuzorota kwa hali ya usalama nchini
Burundi,uimarishwaji wa huduma za kijamii na ukuzaji wa sekta za michezo,utalii
na kilimo ndani ya jumuiya pamoja na mwito kwa viongozi kufuata katiba za nchi
zao
TAFSIRI....“Mgeni yeyote
anayetembele moja ya nchi za Afrika Mashariki aweze kufanya hivyo pasipo
kuulizwa VISA tofauti bali kuwepo na VISA ya aina moja”alisema Willester Simiyu
ambaye ni mshiriki wa zinduka
Mratibu wa “ZINDUKA” Amani Mhinda
amesema mapendekezo yote yatapelekwa kwa Sekretariet na Bunge la jumuiya ya
Afrika mashariki ili yaweze kufanyiwa kazi
Jumuiya ya Afrika Mashariki
inaundwa na nchi za Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi huku kukikadiriwa
kuwepo na wakazi zaidi ya milioni 150 katika ukanda huu.