"BILA UWEKEZAJI TUNAJIDANGANYA" - ASEMA WAZIRI MKUU
Alisema
watendaji serikalini wanapaswa kubadili mitazamo yao hasa wanapokuwa
wanawasiliana na watu wa sekta binafsi kwa sababu kwa mfanyabiashara
yeyote wakati ni mali.
"Tanzania
imejipanga kuelekea kuwa Taifa lenye uchumi wa kati, kama kweli
tunataka kufika huko mapema ni lazima tuwachukulie wadau wa sekta kwa
mtazamo wa tofauti. Siyo anakuja kutaka taarifa unaanza kumzungusha bila
sababu, anataka kusajili kampuni unamwambia unajua mafaili hayaonekani
wakati hakuna cha mafaili wala nini bali unatafuta mwanya wa kudai
chochote," alisema.
Akizungumzia
kuhusu utoaji mikopo kwa ajili ya mitaji ya kibiashara, Waziri Mkuu
aliitaka Taasisi ya Mkoba Equity Fund ihakikishe inajenga kwanza uwezo
wa wahusika ili waweze kuzalisha mali kama ilivyokusudiwa.
Akitoa
mfano wake binafsi, Waziri Mkuu alisema wakati anaanza biashara ya
ufugaji nyuki miaka mitatu iliyopita, hakuwahi kuandaa mchanganuo wowote
(write-up) wala hakuwahi kuandaa mpango wa biashara (business plan).
Matokeo yake, alikuwa anatoa tu fedha mfukoni na kununua vifaa kadri
mahitaji yalivyokuwa yakijitokeza, jambo ambalo alisema si sahihi.
"Ninawasihi
sana viongozi wa Mkoba Equity Fund wasitoe mikopo kwa watu wanaotaka
kufanya biashara kama nilivyoanza mimi. Wekezeni kwanza kwa kuwajengea
uwezo wajasiriamali watakaoomba fedha za mitaji kutoka kwenye taasisi
hii," alisisitiza.
Akitoa
ushauri kwa wajasiriamali wadogo waliotoa shuhuda zao kuhusu changamoto
walizokabiliana nazo wakati wakianzisha biashara zao, Waziri Mkuu
aliwataka wasirudi nyuma wala wasikate tamaa. "Fursa ni nyingi sana na
mnaweza kufanya mambo mengi. Kitu cha msingi ni kuwa na nia thabiti
(determination).
Wajasiriamali
walitoa shuhuda zao ni Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Bi. Teddy
Mapunda; Mkurugenzi wa kampuni ya Go-Financing, Bw. Geoffrey Ndossi,
Mkurugenzi wa kampuni ya SIGA Ltd, Bw. Marwa Busigara na Mkurugenzi wa
kampuni ya WIA, Bw. Eric Mwenda.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.