Header Ads

CCM YAANZA KAMPENI ZA UBUNGE KALENGA KWA KISHINDO, UZINDUZI RASMI FEBRUARI 27, DOKII APAGAWISHA WAPIGA KURA

Mgombea ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa akiwasili kijiji cha Mseke hii leo
Alisindikizwa na viongozi na walinzi wake wa chama

Ilikuwa furaha tele kwa baba yake mdogo Joachim Mgimwa

Niliwapenda walinzi wake jinsi walivyoonekana wakakamavu

Hapa alidhihirisha umma kwamba yeye ni mhehe, mzaliwa wa Iringa na Mtanzania asiye na chembechembe za uzungu kama inavyodaiwa; alicheza ngoma ya asili ya kwao pamoja na wazee hawa

Ilikuwa ni zaidi ya furaha

Dokii aliwanyanyua wananchi kwa kibao chake kinachomsifia Godfre Mgimwa

Nyomi ya kijiji cha Mseke

Wana kwaya nao walitumbuiza kwa nyimbo nzuri za kuisifu CCM na mgombea wao

Kulikuwa na usikivu wa hali ya juu

Katibu wa CCM wa wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu alishusha nondo, akiwaponda Chadema na mgombea wao kwamba wananchi wa jimbo hilo wana Mkataba na CCM mpaka 2015

Naye Katibu wa CCM Songea Mjini, Joseph Ndulango alikuwepo na atakuwepo mpaka siku ya uchaguzi

Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime naye alikuwepo

Katibu wa CCM Bariadi, Miachel Bundara alisema mengi

Huyu ni Elisante Kimaro aliyenogesha mkutano huo kwa kuwataka wananchi wa jimbo hilo kuipondaponda Chadema kwa kura

Omary Mtuwa Katibu wa CCM Maswa naye alishambulia jukwaa

Huyu ni Kitundu Katibu wa CCM Korogwe

Juma Mpeni, Katibu wa CCM Mbinga alitoa nasaha zake kwa wananchi na wapiga kura wa Kalenga

Julius Peter

Mbosa kada maarufu wa CCM

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alizungumzia kwa kirefu kile alichoita kampuni ya Chadema na kwamba si chama cha siasa
Hapa ilikuwa zamu ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu aliyewasihi wana Kalenga kutotoa lift kwa Chadema 


Hawa walikuwa makamanda wa Chadema Kilolo, lakini wamerejea CCM baada ya kukamwata kwenye vurugu wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani lakini viongozi wao walishindwa kuwapa chai walipokuwa mahabusu na nauli baada ya kutoka
Akawapandisha makamanda wa Chadema waliojiunga na CCM hivikaribuni

Mgombea ubunge mwenye alipandishwa kwa mbwembwe kuzungumza na wananchi na kuomba kura
Mimi ni mhehe sio mzungu na kama kila mtu anayeenda kusoma nje ya nchi anakuwa rais wa nchi anayekwenda, basi Chadema watwambie kama hawana wanachama walipata elimu nje ya nchi na kama wapo uraia wao ni wa wapi

Powered by Blogger.