Rukia
Fungameza (20), mkazi wa mtaa wa Ilembo Kata ya Iwambi anashikiliwa na Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutupa chooni kichanga cha kiume na
kusababisha kifo chake.
Mwenyekiti
wa mtaa huo Juma Mbuza alisema Februari 18, mwaka huu walianza kumtilia shaka
mtuhumiwa huyo baada ya kuonekana hana ujauzito huku kukiwa hakuna taarifa
zozote za kujifungua.
Alipoulizwa
kulikoni, mtuhumiwa huyo alidai kajifungua salama huku akiwaondoa hofu majirani
zake.
Tetesi
zilizotilia shaka ujauzito wa mtuhumiwa huyo zilimlazimu Mwenyekiti huyo,
kumtafuta Balozi Daud Dule wa mtaa anaoishi mtuhumiwa huyo ili ajue ukweli wa
tukio hilo.
Alipobanwa,
mtuhumiwa huyo alikiri kujifungua salama lakini Februari 18 alilazimika kukitupa kichannga
chake chooni kwa kuwa mimba haikuwa ya mme anayeishi naye.
Baada
ya kukiri kufanya unyama huo, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi na kufikishwa
kituo cha Polisi Iyunga.
Baadhi
ya mashuhuda akiwemo mama Emilly Amoni na Paulo Mbawala wamelaani vikali
kitendo kilichofanywa na mwanamke huyo kwani wamedai ni cha kinyama na ni cha
kwanza mtaani kwao hivyo wanaomba sheria iweze kuchukua mkondo wake ili
kukomesha kabisa vitendo vya kikatili vya aina hiyo.
Na
Ezekiel Kamanga
Mbeya
yetu
|