Header Ads

MAMA SAMIA AWATAKA WANAWAKE KUWA KITU KIMOJA KULINDA HAKI ZAO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amelaani na kukemea vikali vitendo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinavyoendelea katika jamii na amewataka wananchi kote nchini kushirikiana katika kukabiliana na vitendo hivyo nchini.


Makamu wa Rais Mhe Samia amesema vitendo hivyo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinamchukiza sana hivyo ametoa wito maalum kwa wananchi na wadau wote bila kujadili dini, kabila wala rangi kupambana ipasavyo na vitendo hivyo ambavyo vinarudisha nyuma jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.

Kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani,Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anafurahishwa na hatua na jitihada zinazochukuliwa na wanawake kote nchini katika kujikwamua kiuchumi kwa kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali katika kuelekea katika uchumi wa viwanda.

Amesema jukumu kubwa la serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanawake wanaboreshewa mazingira ipasavyo  ya kufanyia kazi, hasa shughuli za ujasiriamali ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

Katika uundaji wa majukwaa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini, Makamu wa Rais Hassan amesema kazi hiyo inaendelea vizuri na kutaka mikoa na wilaya ambazo bado haijaunda majukwaa hayo kufanya hivyo haraka iwezekanavyo. 
Powered by Blogger.