TASWIRA ZA MASHABIKI WA ARSENAL WAKIMFUKUZA WENGER WALIYEMCHOKA
Subira “sugu” ya mashabiki wa Arsenal inaonekana imefikia ukomo.
Baada ya kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Bayern Munich safari hii wakiwa nyumbani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashabiki wake wamefanya maandamano kiana wakiwa na mabango yanayomfukuza Kocha Arsene Wenger.
Wengi wamekuwa wakisisitiza Wenger aondoke na kama imeshindikana, suala la mkataba mpya wanaona haitakuwa sawa.
Mashabiki hao wanaonekana kuchoshwa na wana hasira kwelikweli, lakini Wenger kama kawaida yake, yuko kimyaaa.