Header Ads

LA LIGA: LEO RONALDO KIKOSINI WAKITEGEMEA KIFUNGO KUFUTWA!

>>JUMAMOSI: REAL v ELCHE!
RONALDO-FURAHAKOCHA wa Real Madrid Carlo Ancelotti anaamini Adhabu ya Kufungiwa Cristiano Ronaldo Mechi 3 Leo itapunguzwa na kubaki Mechi 2 na Leo hii kuweza kucheza Mechi ya La Liga dhidi ya Elche Uwanjani Santiago Bernabeu.
Ancelotti amemuweka Ronaldo kwenye Kikosi chake cha Wachezaji 20 kwa Mechi hii ya Leo.
Tayari Ronaldo ameshatumikia Kifungo cha Mechi mbili baada kupewa Kadi Nyekundu walipotoka Sare 1-1 na Athletic Bilbao hapo Februar1 2 na ushindi kwa Real hii Leo utawafanya wakae kileleni japo kwa muda kwa vile Barcelona wanacheza baadae Usiku huu Ugenini na Real Sociedad.
Rufaa mbili za Real kupinga Adhabu ya Ronaldo zilitupwa na Real sasa wanategemea Baraza la Michezo la Spain, CSD, kusikiliza Rufaa yao ya mwisho hii Leo.
Mbali ya Ronaldo, pia Real itamkosa Luka Modric ambae na yuko Kifungoni kwa Mechi 1 baada kujizolea Jumla ya Kadi za Njano 5.
Ili kuziba pengo la Modric, Carlo Ancelotti, amedokeza kuwa Asier Illarramendi atacheza Mechi hii.
Wikiendi hii La Liga imeingia Raundi ya 25 na juu kileleni wapo Mabingwa Watetezi FC Barcelona, wakifuatiwa na Real Madrid na Atletico Madrid lakini zote hizi zimefungana kwa Pointi, wote wakiwa na Pointi 60 kila mmoja, na kutenganishwa kwa ubora wa Magoli kitu ambacho mwishoni mwa Msimu hakihesabiki.
Kwa Kanuni za La Liga, mwishoni mwa Msimu, ikiwa Timu zimefungana kwa Pointi kinacho watenganisha ni Matokeo yao Mechi zao za Uso kwa Uso.
Raundi ya 25 ilianza Jana Usiku kwa Mechi kati ya Real Valladolid na Levante ambayo ilimalizika 1-1.
Leo Jumamosi, FC Barcelona wako Ugenini kucheza na Real Sociedad Mjini San Sebastian Uwanjani Anoeta ambako Barca hawajashinda katika Mechi 5 Uwanjani hapo.
Mara ya mwisho Timu hizi kucheza ni mapema Mwezi huu kwenye Nusu Fainali ya Copa del Rey ambako walitoka 1-1 Uwanjani Anoeta na Barca kusonga Fainali kwa vile walishinda 2-0 Nou Camp katika Mechi ya kwanza.
Nao Atletico Madrid watacheza Jumapili Ugenini na Osasuna ambayo iko Nafasi ya 14.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Ijumaa Februari 21
Real Valladolid 1 Levante 1
Jumamosi Februari 22
1800 Real Madrid CF v Elche CF
2000 Celta de Vigo v Getafe CF
2200 Real Sociedad v FC Barcelona
2359 UD Almeria v Malaga CF
Jumapili Februari 23
1400 Rayo Vallecano v Sevilla FC
1900 Real Betis v Athletic de Bilbao
2100 Valencia v Granada CF
2300 Osasuna v Atletico de Madrid
2359 RCD Espanyol v Villarreal CF
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
FC Barcelona
24
19
3
2
69
17
52
60
2
Real Madrid CF
24
19
3
2
68
24
44
60
3
Atletico  Madrid
24
19
3
2
59
16
43
60
4
Athletic de Bilbao
24
13
5
6
43
30
13
44
5
Villarreal CF
24
12
4
8
44
29
15
40
6
Real Sociedad
24
11
7
6
43
34
9
40
7
Sevilla FC
24
8
8
8
42
41
1
32
8
Valencia
24
9
5
10
36
35
1
32
9
RCD Espanyol
24
9
5
10
28
30
-2
32
10
Levante
24
8
8
8
23
30
-7
32
11
Celta de Vigo
24
8
5
11
31
35
-4
29
12
Granada CF
24
8
3
13
21
30
-9
27
13
Elche CF
24
6
8
10
22
34
-12
26
14
Osasuna
24
7
5
12
21
37
-16
26
15
Getafe CF
24
7
4
13
22
39
-17
25
16
UD Almeria
24
7
4
13
24
42
-18
25
17
Malaga CF
24
6
6
12
23
34
-11
24
18
Real Valladolid
24
4
9
11
26
42
-16
21
19
Rayo Vallecano
24
6
2
16
25
58
-33
20
20
Real Betis
24
3
5
16
20
53
-33
14
Powered by Blogger.