Watu wenye uwezo watakiwa kuisaidia Serikali Kupambana Na Umasikini
Watu wenye uwezo wa kifedha
wameaswa kujitoa kuisaidia serikali katika kupambana na janga la umasikini
nchini ikiwa pamoja na kuwainua kiuchumi baadhi ya wananchi wasiojiweza
kimaisha.
Rai hiyo imetolewa katika hafla
ya kuwatunuku shahada ya uzamivu baadhi ya watendaji wa serikali pamoja na
Baadhi ya watu wanaofanya kazi kiroho iliyofanyika Jijini Mwanza.
Chuo cha Africa Graduate
University, makao makuu yake nchini Sierra
Leone limejikita mkoani Mwanza Kutunuku vyeti Vya heshima shahada ya Udokta
Kufanya kazi kwa weledi kwa
watumishi wa Serikali , kusaidia jamii katika masuala mbalimbali pamoja na kazi
za kumtumikia Mungu ndio nguzo kuu kwa chuo hiki.
Ambapo wahitimu 10 wametunukiwa vyeti
kutoka serikalini pamoja na wachunguji
ikiwa ni sehemu ya kuonesha Heshima na Uthamini
wa juhudi ya kuihudumia jamii.
Kutunukiwa kwa vyeti hivyo
inaashiria tayari wanashahada ya udaktari katika kuwajibika vyema kwa nafasi
zao
Awali katika hafla hivyo Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo Shabaha yake ni umuhimu wa vyeti hivyo kutia
moyo watumishi na kuwajibika Ipasavyo.
Baadhi ya watunukiwa wanabainisha
uhalali wa kutunukiwa vyeti na chuo hicho huku kilio chao kikibaki kwa tu wenye
uwezo nao kujitoa kusaidia jamii katika masuala mbalimbali.
Hafra hiyo imehudhuriwa na
viongozi Mbalimbali wa kidini na serikali