Zaidi watu 1,000 warejea kwenye tiba mkoani Sngida Kupunguza Makali Ya Vvu
ZAIDI ya watu elfu moja wanaoishi
na Virusi vya ugonjwa wa UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani
Singida, wamerejea kwenye tiba baada ya kuacha kabisa kuhudhuria Kliniki maalum
za kuwahudumia miaka mitatu iliyopita kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu za kuacha dawa za kufubaza
Virus zinatajwa kuwa ni Kikombe cha Babu wa Loliondo, unyanyapaa na wengine
kudhani kuwa wamepona hivyo kuendelea kudhofika hadi walipofikiwa na mpango wa
huduma majumbani unaoendesha na Shirika la SEMA Singida na kurejeshwa kwenye
tiba.
Siku chache baada ya Serikali
kusitisha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Dunia, yaliyopangwa kufanyika Kitaifa
mkoani Singida mwaka huu, Shirika la SEMA-Singida linalojishughulisha na
mapambano dhidi ya ugonjwa huo, limejitokeza kuelezea mafanikio ya mradi wake
wa huduma majumbani.
Zipo sababu zinazotajwa kuchangia
baadhi ya watu kuacha kutumia dawa za kufubaza virusi vya UKIWMI ikiwemo garama
za kununulia dawa.
Baadhi ya watu wanaoishi na
Virusi vya UKIMWI wameleza maisha yao ya awali na jinsi mpango huo wa huduma
majumbani ulivyosaidia kuboresha maisha na kupunguza unyanyapaa katika jamii.
Chini ya mpango huo unaofadhiliwa
na Mradi wa Tunajali, tangu mwaka 2012 zaidi ya shilingi milioni 300 zimetumika
kutoa huduma majumbani kwa watu 1,705 wanaoishi na virusi vya UKIMWI Wilayani
Iramba.