Wachimbaji wadogo watano wafariki Geita
Wachimbaji wadogo watano
wamefariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi katika maeneo ya Mgusu na Nyanza mkoani
Geita.
Matukio hayo yametokea
kwa nyakati tofauti ambapo wachimbaji kumi waliingia eneo la Nyanza majira ya
saa tisa novemba 28 na wakiwa katika harakati za uchimbaji wakaangukiwa na
kifusi huku usiku wa novemba 29 tukio hilo limetokea mgusu na kusababisha
wachimbaji hao kufariki.
Maeneo ya Nyanza na
Mgusu wanayoingia wachimbaji wadogo kwa ajili ya kujitafutia dhahabu yako chini
ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita.
Wachimbaji hao
wanasema tukio la kufukiwa kwa wenzao wa mgusu walipata taarifa usiku wa saa
sita ndipo walipotoa taarifa kwa wenzao na kuanza zoezi la uokoaji ambapo
walifanikiwa kutoa miili.
Waliofariki ni
Emanuel Emanuel,Luca Deus,Maliatabu Budonyanga,Clement Richard na Baraka
Katunzi ambaye bado walikuwa wanafanya jitihada za kumtafuta.
Zoezi la uokoaji
limefanyika kikamilifu asubuhi na kufanikiwa kuoa maiti nne huku mmoja akiwa
bado anatafutwa katika kifusi hicho.
Wachimbaji hawa
ambao wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuingia maeneo ambayo ni hatarishi
ambapo novemba 28 eneo la nyanza majira ya mchana walifukiwa wachimbaji kumi
lakini kwa juhudi za mgodi wakafanikiwa kutolewa wakiwa hai.
Vijana hawa wamedai
kujihatarishia maisha kutokana na kukosa ajira na njia pekee wanayoitegemea ni
uchimbaji kwahiyo huwa wanangalia eneo rahisi linalopatikana dhahabu na kwenda
kuanza kuchimba.
Wachimbaji hawa
wadogo hawako rasmi jambo ambalo limekuwa gumu kuwawezesha kwa pamoja na
kuwataka wafuate taratibu kwani serikali inafanya jitihada za maeneo kwa ajili
ya wachimbaji.