Header Ads

WENGER ALAUMIWA KUUMIA KWA ALEXIS SANCHEZ

Sanchez-injury
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametupiwa lawama na wadau wa klabu ya Arsenal akiwemo gwiji Thierry Henry kutokana na kumchezesha mchezaji Alexis Sanchez katika mchezo wa jana dhidi ya Norwich na kumsababishia aumie na kutolewa nje kabla mechi haijaisha.

Alexis Sanchez alipata majeraha madogo katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Dinamo Zagreb katikati ya wiki, lakini Arsene Wenger alitamka kuwa Sanchez angekua fiti kucheza mechi ya jana, lakini baada ya kucheza aliumia na kutolewa nje na sasa anaongeza idadi kubwa ya majeruhi iliyopo katika kikosi cha Arsene Wenger.
Legendari Thierry Henry alimlaumu kocha huyo kwa kutochukua tahadhari kwa kumuacha nje mchezaji huyo huku akienda mbali zaidi na kusema kuwa Sanchez alitakiwa kutomaliza mchezo dhidi ya Dinamo Zagreb ulioisha kwa Arsenal kushinda goli 3-0 ili aweze kumpumzisha.
Kuumia huko kwa Alexis Sanchez ni habari mbaya kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal ambao wanashuhudia timu yao ikiwa na wimbi kubwa la majeruhi ambapo kiungo Coqueline aliumia wiki iliyopita na kujumuika na majeruhi wa muda mrefu Jack Wilshere, Danny Welbeck na Thomas Rosicky huku pia Mikel Arteta na Theo Walcott wakiwa majeruhi.
Powered by Blogger.