NGULI MAN UNITED WAKUBALIANA DILI KUINUNUA KLABU SALFORD CITY
NI ‘CLASS OF 92’: GARY & PHIL NEVILLE, GIGGS, SCHOLES & NICKY BUTT!
WACHEZAJI
NGULI wa Manchester United, Gary Neville, Phil Neville, Ryan Giggs,
Paul Scholes na Nicky Butt wamefikia makubaliano kuinunua Klabu ya
Salford City.
Dili hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Msimu baada ya kupata baraka za FA, Chama cha Soka England na Wasimamizi wa Ligi.
Salford City ipo kwenye Ligi ya Evo-Stik
Daraja la Kwanza huko Kaskazini mwa England Maeneo ya Jiji la
Manchester na Uwanja wake upo Moor Lane huko Kersal.
Wachezaji hao wa zamani wa Man United wote chimbuko lao ni Maeneo ilipo Salford City.
Hivi sasa Ryan Giggs ni Kocha Mchezaji
wa Man United, Phil Neville ni Kocha Msaidizi Man United chini ya David
Moyes, Nicky Butt anafundisha Timu ya Vijana ya Man United wakati Gary
Neville ni Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya England na pia ni
Mchambuzi wa Soka kwenye Kituo cha TV cha Sky Sports.
Wakiongea kuhusu Salford City Wachezaji
hao walitamka vitu mbalimbali na Gary Neville alisema: “Nilifanya
majaribio yagu ya kwanza na Manchester United huko Salford nikiwa na
Miaka 11 na sitasahau umuhimu wake!”
Paul Scholes amesema: “Tunajua ni ngumu lakini tuna nia na tuna plani nyingi hapo!”
Butt amesema: “Eneo hilo lina historia ya Miaka 320 nyuma na ni lazima lilindwe!”
Phil Neville: "Ni muhimu kulinda kazi ngumu iliyofanyika kwenye Ligi za chini!”
Giggs said: "Kila Mtu anajua umuhimu wa Salford kwangu mimi!”
Nae Mwenyekiti wa Salford City, Karen Baird, amesema huu ni wakati wa furaha kwao kwani utaleta mafanikio makubwa kwao.
Akithibitisha Dili hii kwenye Mtandao
wa Twitter, Gary Neville, aliwahakikishia Wadau kuwa Dili hiyo
haimanishi kubadilishwa Jina Salford City wala Uwanja wake wala
Menejimenti yake kama ilivyokuwa hulka ya Siku hizi kwa Wamiliki wapya
wa Klabu