WAZIRI MUHONGO AZOMEWA SOKO LA WAKULIMA KAHAMA,WANANCHI WAPAZA SAUTI WAMUITA MWIZI! MWIZI! MWIZI!......
Waziri
wa nishati na madini Mhe.Sospeter Muhongo amejikuta katika wakati mgumu
na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la wakulima katikati
ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini wilayani Kahama
mkoani Shinyanga.
Tukio
hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara wake wakitokea kata
ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya Bulige jimbo la Msalala
kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na wakala wa umeme
vijini nchini (REA) unaoendelea kufungwa katika maeneo mbalimbali wilayani
humo.
Baada
ya kufika katika eneo hilo wananchi hao walianza kumzomea wakidai ni “mwizi wa
fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kelele ambazo
ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona anayezomewa ni waziri
yupi.
Hata
hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri huyo ambaye yuko ziara
kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali katika eneo hilo la soko
la wakulima wakijadili hatima yake katika mpango mzima wa mgogoro wa uchotwaji
wa mabililioni ya shilingi kwenye akaunti hiyo ya Escrow.
Pamoja
na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake wilayani Kahama ameacha
neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu baada ya kuwaahidi umeme katika
awamu ya tatu ya mradi ya nishati vijijini.