Header Ads

AFRIKA NA 5 ZA BRAZIL: LEO NIGERIA, IVORY COAST KUKATA TIKETI?

LEO NI NIGERIA v ETHIOPIA, SENEGAL v IVORY COAST!!
SENEGAL WAKO ‘NYUMBANI CASABLANCA, MOROCCO’!!!

BADO GEMU 5 zimebaki na bado Afrika kujua Timu zao 5 za kwenda Brazil Mwezi Juni 2014 kucheza Fainali za Kombe la Dunia na leo mbili za kwanza zitapatikana baada ya Mechi mbili za leo.
PATA UTAMU:


AFRIKA
RATIBA:
Marudiano:
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumamosi Novemba 16
18:00 Nigeria v Ethiopia [2-1]
22:00 Senegal v Ivory Coast [1-3]
Jumapili Novemba 17
17:30 Cameroon v Tunisia [0-0]
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]
**FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
...................................................................................................
DROGBA-IVORY_COASTEthiopia wanasafiri kwenda Nigeria kujaribu kupindua kipigo cha Bao 2-1 walichopewa huko kwao Addis Ababa na Mabingwa wa Afrika Nigeria Mwezi Oktoba na leo wapo Mjini Calabar kujaribu kutimiza hilo na kupata Tiketi ya kwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Mechi nyingine ya leo itachezwa huko Casablanca, Morocco kati ya ‘Wenyeji’ Senegal ambao nao wanasaka kupindua kichapo cha 3-1 walichopewa na Ivory Coast katika Mechi ya kwanza.
Senegal wanalazimika kucheza nje ya Nchi yao Mechi zao za Nyumbani baada ya kufungiwa kutokana na vurugu Uwanjani.
Ethiopia, chini ya Kocha Sewinet Bishaw, imemrudisha Kikosini Straika wao Getaneh Kebede anaecheza huko Afrika Kusini baada ya kuikosa Mechi ya kwanza na Nigeria kufuatia kuumia Goti.
Bosi wa Nigeria, Stephen Keshi, amemwita kundini Beki Kenneth Omeruo pamoja na Kipa anaedakia Nchini Ufaransa Vincent Enyeama huku Rueben Gabriel, Chigozie Agbim, Francis Benjamin, Solomon Kwambe, Azubuike Egwuekwe na Sunday Mba wakiendelea kubaki kwenye Timu.
Akielezea Mechi ya leo, Stephen Keshi, amesema: “Gemu ya leo na Ethiopia ni muhimu kwa Nchi na Wachezaji wote wanajua hilo!”
Ivory Coast, chini ya Kocha Sabri Lamouchi, wanahitaji kulinda ushindi wao wa Bao 3-1 dhidi ya Senegal ili waende Brazil, lakini tayari wana upungufu kwenye Kikosi chao.
Kwenye Mechi hii na Senegal, Ivory Coast itawakosa Boka Arthur wa VfB Stuffgart, Siaka Tiene wa Montpellier, ambao ni Majeruhi, pamoja na Cheick Tiote wa Newcastle ambae yupo Kifungoni baada ya Kadi.
Senegal, ambao wamelazimika kuchezea Mechi zao za Nyumbani Nchini Morocco baada ya Mashabiki wao kuleta fujo Uwanjani Mwezi Oktoba 2012 walipocheza Mechi ya AFCON na Ivory Coast Mjini Dakar, wameendelea kumpiga chini Straika wa Chelsea Demba Ba na pia kumuacha Beki wa Marseille Souleymane Diawara.
Lakini miamba wengine, kama vile Zarko Toure, Mame Birame Diouf na Pape Kouly Diop, bado wapo kwenye Timu.
..................................................................................
TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL
[Jumla 21 Bado 11]:
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA
**FAHAMU:
- DROO YA KUPANGA MAKUNDI:
-KUFANYIKA TAREHE 6 DESEMBA 2013 Costa do Sauípe Resort, Mata de São João, Bahia, Brazil
-Kwenye Droo hiyo Timu 7, pamoja na BRAZIL, ambazo ziko juu kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani zitawekwa Chungu Na 1 na Timu nyingine 24 zilizobakia zitagawanywa nane nane na kuingizwa Vyungu vingine vitatu na kutenganishwa kutoka Mabara zinakotoka.
-FAINALI KUCHEZWA: 12 Juni 2014 hadi 13 Julai 2014
///////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////
Powered by Blogger.