Header Ads

wananchi wataka korosho iuzwe mkono kwa mkono na si kwa mkopo



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kata ya Mbesa ,kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Ruvuma ambayo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Mbesa, kijiji cha Mbesa juu ya mpango wa serikali katika kuhakikisha wananchi hao wanapata maji,Kushoto Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma kitabu kinachoonyesha Mbesa ipo kwenye mpango wa kupata maji.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk Asha-Rose Migiro  kujenga daraja la mto Munjapu wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi barabara itakavyokuwa baada ya kukamilika kwa daraja la mto Munjapu,lililopo kijiji cha Mnemasi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama,kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika mkoa wa Ruvuma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.(P.T)
Powered by Blogger.