WOJCIECH SZCZESNY ASAINI DILI MPYA ARSENAL!
NI MKATABA WA MUDA MREFU AMBAO HAUKUTAJWA!
KIPA kutoka Poland Wojciech Szczesny amesaini dili mpya Klabuni kwake Arsenal itakayomweka kwa muda mrefu zaidi.
Msimu huu, Wojciech Szczesny ameisaidia
sana Arsenal kufanya vizuri na hata kuwa inaongoza Ligi Kuu England kitu
ambacho kimeleta matumaini kwamba wanaweza kutwaa Ubingwa Msimu huu.
Akithibitisha habari hizi, Meneja wa
Arsenal, Arsene Wenger, amesema: “Tumefurahi Wojciech amesaini Mkataba
wa muda mrefu. Siku zote nilikuwa naamini yeye ni Mchezaji mwenye
Kipaji, mwenye uwezo mzuri na mwenye nguvu kiakili. Anaendelea kukua na
kuwa bora zaidi kila wakati. Atakuwa ni sehemu muhimu kwa Arsenal kwa
Miaka mingi ijayo.”
Szczesny, mwenye Miaka 23 na ambae
alijiunga na Arsenal Mwaka 2006 akitokea Legia Warsaw ya Poland,
amesema: “Nimefurahi sana kusaini Mkataba mpya. Arsenal ni kama Familia
yagu na nimefurahi nitabaki hapa kwa muda mrefu.”
Hata hivyo, hakuna alietoboa Dili hiyo ya muda mrefu ni Miaka mingapi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 23 Novemba
1545 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Southampton
1800 Fulham v Swansea City
1800 Hull City v Crystal Palace
1800 Newcastle United v Norwich City
1800 Stoke City v Sunderland
2030 West Ham United v Chelsea
Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United
Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
11 |
12 |
25 |
2 |
Liverpool |
11 |
11 |
23 |
3 |
Southampton |
11 |
10 |
22 |
4 |
Chelsea |
11 |
8 |
21 |
5 |
Man Utd |
11 |
5 |
20 |
6 |
Everton |
11 |
4 |
20 |
7 |
Tottenham |
11 |
3 |
20 |
8 |
Man City |
11 |
16 |
19 |
9 |
Newcastle |
11 |
-1 |
17 |
10 |
West Brom |
11 |
0 |
14 |
11 |
Aston Villa |
11 |
-1 |
14 |
12 |
Hull |
11 |
-5 |
14 |
13 |
Swansea |
11 |
0 |
12 |
14 |
Cardiff |
11 |
-6 |
12 |
15 |
Norwich |
11 |
-12 |
11 |
16 |
West Ham |
11 |
-2 |
10 |
17 |
Stoke |
11 |
-4 |
10 |
18 |
Fulham |
11 |
-9 |
10 |
19 |
Sunderland |
11 |
-14 |
7 |
20 |
Crystal Palace |
11 |
-15 |
4 |