MeTL yazindua show ya mwaka kwa watoto na vijana
Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akizungumza na waandishi wa
habari juu ya umuhimu wa kusaidia jamii kupitia (Corporate Social
Responsibility) kama njia mojawapo ya kupiga vita umaskini katika nchi
za bara la Afrika. Kushoto kwake ni Meneja Mkuu Ledger
Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi, Kulia ni Afisa Uhusiano wa Kampuni
ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi na Kushoto ni Irfaan Jaffer kutoka
MeTL.
.Lengo la maonyesho ni kusaka vipaji miongoni mwa vijana
.Kuanzia siku ya Krimasi hadi Boxing day zawadi mbalimbali na Tsh m kushindaniwa
Na Damas Makangale
KAMPUNI
YA MOHAMMED ENTERPRISES (MeTL) Tanzania kwa kushirikiana Ledger Plaza
Bahari Beach wamezindua maonyesho ya elimu ya mwaka kwa watoto nchini
yenye kushindaniwa zawadi mbalimbali na mshindi wa jumla kujinyakulia
fedha taslimu Tsh5m.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye hoteli ya Ledger
Plaze Bahari Beach Hotel, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Bi Fatema
Jaffer, amesema kampuni ya Metl ina jail maslahi ya wateja wake na
watanzania kwa kupitia dhana ya Kusaidia Jamii na Kujenga mahusiano
(Corporate Social Responsibility) kwa kusaidia kuinua vipaji vya watoto.
“Kwenye
maonyesho haya ya wazi ya kutazama vipaji mbalimbali vya watoto hasa
kwenye elimu tumeamua kudhamini maonyesho haya ili kusaidia jamii kuweza
kukuza vipaji vyao vya manufaa yao binafsi na jamii kwa ujumla,”
amesema.
Bi.
Jaffer amesema kuwa katika taifa la Tanzania kuna vipaji vingi hasa kwa
vijana na watoto lakini wanakosa msukumo na jamii kuwatia moyo ili
vipaji vile viweze kufanya kazi kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
Amesema maonyesho hayo yataanza rasmi kuanzia tarehe 25th,
26 na 27 kwenye viwanja vya Ledger Plaze Bahari Beach yenye dhumuni ya
kugundua, kutambua kuendeleza, kutia moyo na kupapanua vipaji vya watoto
vilivyojivicha kwenye jamii ya watanzania.
Meneja
Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo ya watoto na vijana katika
kuonyesha vipaji vyao mbalimbali.
Bi.
Jaffer amesema maonyesho hayo yanaitwa (MO KIDS GOT TALENT) kwa sababu
mdhamini mkuu ni Metl na watakuwa tayari kufanya kazi bega kwa began a
watoto, vijana na wazazi wao katika kutambua, kuendeleza na kukuza
vipaji vya watoto kupitia maonyesho haya.
Kwa
upande wake Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Wissem Souifi,
amesema maonyesho hayo ni jukwaa pekee kwa vijana na watoto wa Tanzania
kuonyesha vipaji vyao mbalimbali katika elimu na Nyanja nyingine za
kuburudisha.
“Maonyesho
haya yatawajenga vijana kuwa na ujasiri na kuzalisha watu wenye
mafanikio mbalimbali katika maisha na kusukuma gurudumu la maendeleo
mbele,” amesema.
Amesema
kuwa katika maonyesho hayo wazazi wanaombwa kuwaruhusu watoto wao
waende kwenye tamasha hilo kubwa na la kipekee kuandaliwa na makapuni
makubwa hapa nchini.
Afisa
Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi, akihamasisha
wazazi nchini kuruhusu watoto wao wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe
25, 26 na 27 mwezi Desemba ambapo watoto 100 wa kwanza kujisajili
wataingia bure.
Kisura
na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo akielezea umuhimu wa tamasha
hilo kubwa la Elimu kwa Vijana na manufaa ya kusaka vipaji kwenye umri
mdogo ambapo pia amewataka wazazi kuwapa ushirikiano wa kukuza vipaji
vya watoto wao.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer kwenye picha ya pamoja na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Frost Africa, Bi.Lilian Ngowi pamoja na Kisura na Balozi wa MO Beauty Soap Jokate Mwegelo.
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi, Mkurugenzi
wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, Meneja Masoko Msaidizi wa
MeTL Group, Bw. Aunali Bandali, Irfaan Jaffer kutoka MeTL Group pamoja
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fros Africa, Bw. Peter Sekasiko.
Meneja Mkuu wa Ledger Plaza Bahari Beach, Bw. Wissem Souifi akimtembeza
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer maeneo mbalimbali
ya hoteli hiyo.