Header Ads

BREAKING NEWS:Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi YATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015,SASA WENYE DIVISION FOUR YA 32 HADI 34 RUKSA KUAPPLY


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatangaza nafazi za Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Cheti kwa Mwaka wa Masomo 2014/2015.
TANGAZO LA MAFUNZO YA UALIMU CHETI -2014 (146.88 kB)

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 UTANGULIZI








  1. Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
  2. Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
  3. Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
  4. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
  5. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz);
  6. Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
  7. Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)






  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na MonduliMwombaji awe amehitimu: Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.
  2. Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Klerruu. Mwombaji awe amehitimu:



  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango cha ‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi Jamii.
  2. Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara.
  3. Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika chuo cha Butimba. Mwombaji awe: Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja



  1. Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpwapwa, Tukuyu, Songea, Butimba, Klerruu na Monduli.Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  2. Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda, Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa, Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Sayansi Jamii; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  3. Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga, Kasulu. Mwombaji awe: Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya Biashara; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
  4. Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi. Mwombaji awe: Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili, Au Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.




  1. Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
  2. Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile anachokipendelea zaidi;
  3. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
  4. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz), OWM-TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
  5. Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
  6. Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: www.moe.go.tz, OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu;




Powered by Blogger.