Header Ads

Hii inashangaza Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?

140512084113 placenta b4b77
Na Hudugu Ng'amilo
140512084111 mtoto 753dc
Njia za kula Kondo la Nyuma

Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.


'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.

Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda
Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa na Bakteria ambayo inaweza kusababisha athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo la nyuma.
Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading, anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie''
"nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo nilijidharau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata nguvu na kupona haraka,'' alisema mama Charlie.
140512090319 kondo yakaangwa 512x288 bbc nocredit 75ea9
'Kondo la Nyuma ni nini?'

Baadhi ya wanawake huikausha na kuikaanga kama nyamaHii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na kitovu.Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa upasuaji.Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama wengine wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya magharibi.'Je wanasayansi wanasemaje?'Hadi leo hakuna utafiti wowote kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.CHANZO BBC
Powered by Blogger.