Inasikitisha Sana,Tazama Picha ya mwanamke aliyepiga magoti hospitali kubembeleza apatiwe dawa za maumivu kabla ya kifo chake.
Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa hadi kuamua kupiga magoti hospitali akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na kuzidiwa kwake lakini wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti ulimkuta.
Siku mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama huyo Margaret Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika kumzidi kutokana na kushindwa kupatiwa msaada.
Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E North Staffordshire nchini Uingereza na wanafamilia yake akiwa na maumivu makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu.