KAKA WA MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI NAYE APOTEA
Vipimo
Mbali na tiba, Nasra pia alifanyiwa usafi wa mwili wake ambao ulikuwa mchafu kutokana na kutoogeshwa kwa muda mrefu na sasa inaelezwa kuwa yuko kwenye hali ya kuridhisha na wasamaria wema wameanza kujitokeza kumpa misaada ya nguo na chakula.
REJEA
Nasra aligundulika akiwa amewekwa katika boksi nyumbani kwa mama yake mkubwa, Mariamu Said, mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro aliyekuwa akimlea. Hivi sasa, Mariam pamoja na mumewe, Omar Mtonga wanashikiliwa na polisi kwa kumficha mtoto wa huyo kwenye boksi kwa miaka minne. Mama yake Nasra alifariki wakati mwanaye huyo akiwa na umri wa miezi tisa.