Header Ads

KAMBI YA UPINZANI WASUSIA KUJADILI BAJETI YA NISHATI NA MADINI

Habari zilizopatikanahivi punde zinasema, wabunge wanaounda kambi ya rasmi ya upinzani Bungeni wamesusiamjadala unaoendelea jioni hii kwa kile walichodai kuwa mkakati uliopangwa nawenzao wa CCM kujaribu kufunika madudu yaliyogubika ufujaji wa fedha za IPTL.Akizungumza muda mfupikabla ya kutoka nje ya Bunge, Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alisemakuna kila dalili kwamba wabunge wa CCM walishakaa kikao kabla ya kuanzakujadili Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwamba wahakikishewanasambaratisha kila hoja inayohusiana na suala zima la kampuni ya ufuajiumeme ya IPTL.Mbowe alimshutumu Spikana wabunge wa CCM kujaribu kufifisha hoja za wapinzani waliosisitiza kutakasuala hilo lijadiliwe kwa kina na bila kutanguliza misimamo ya vyama vyao.“Mheshimiwa Spika, humundani ni dhahiri kuna wabunge tayari wameingia na misimamo ya vyama vyao bilakujali suala hili ni zito sana kwa mustakabali wa taifa letu. Najua humu ndanimpo wengi kuweza kupitisha msimamo wenu kuhusu suala hili, lakini najuamtahukumiwa huko nje siku moja mbeleni,” alisema Mbowe.Akahitimisha kwa kusema, “Ilituwe na amani, naomba tuwaache muendelee kujadili wenyewe (CCM) suala hili kwaamani kabisa.”Kauli hiyo ikazushakelele kutoka kwa wabunge wanaomanika kuwa wa chama tawala cha CCM wakirushamaneno ya kejeli wakati  wabunge wa kambiya upinzani wakitoka nje ya bunge majira ya Saa 10:30 jioni hii.Mapema kabla, WaziriKivuli wa wizara hiyo, John Mnyika akisoma Bajeti Mbadala ya kambi hiyoalielekeza shutumu nzito dhidi ya ufisadi uliokithiri kwenye suala zima lafedha ilizolipwa IPTL, ambapo alimwomba Spika wa Bunge, Anne Makinda kuundakamati maalum ya Bunge kuchunguza suala hilo.Wabunge wa kambirasmi ya upinzani wanatoka katika vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi.
Powered by Blogger.