Majambazi yatikisa Shinyanga mjini!! YAUA MFANYABIASHARA KWA RISASI NA KUPORA PESA ,SIMU NA VOCHA KWA MFANYABIASHARA MWINGINE
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Evarist Mangalla |
Mfanyabiashara
mmoja aliyejulikana kwa jina Kulwa Cosmas(42) mkazi wa eneo la Ndala
mjini Shinyanga akiwa nyumbani ameuawa kwa kupigwa risasi moja ya
shingoni baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Tukio hilo limetokea jana saa moja na nusu usiku katika eneo la Ndala mjini Shinyanga.
Kamanda wa jeshi la polisi
mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Evarist
Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
Kamanda Mangalla amesema tayari jeshi la polisi linawashikilia watu wanne kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
Amewataja
watu hao kuwa ni Haudax James(36) mkazi wa Tambukareli mjini
Shinyanga,Pirima Gwiliza(43) mkazi wa Tambukareli mjini Shinyanga,Paulo
Masalu(31) mkazi wa Ngokolo mjini Shinyanga pamoja na Ramadhan Juma(45)
mkazi wa Kitangiri mjini Shinyanga .
Siku
hiyo hiyo ya jana mwanamme aitwaye Yahaya Mrisho(46)ambaye pia ni
mfanyabiashara mkazi wa kata ya Ibinzamata katika manispaa ya Shinyanga
amevamiwa nyumbani kwake na watu
wasiojulikana wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha aina ya
SMG kisha kumpora pesa taslimu 300,000/= ,vocha za simu zenye thamani ya
shilingi 150,000/= pamoja na simu 4 za mkononi zisizojulikana thamani
yake.
Kamanda
Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali na kwamba mpaka
sasa hakuna mtu aliyeshiliwa na jeshi la polisi na ametoa wito kwa
wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wa tukio
hilo.