Header Ads

HII KALI..!! TAIRI YA TREKTA YAPASUKA NA KUUWA MTU KWA UPEPO WILAYANI KAHAMA

Mkazi wa kata ya kagongwa Makonda Sita (28) amefariki dunia baada ya tairi ya Trekta aliyokuwa akijaza upepo kupasuka katika kijiji cha kagongwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisa mtendaji wa kata ya Kagongwa Shaban Abas, Makonda aliangizwa kwenda kujaza tairi upepo na mmiliki wa Trekta hiyo Habib Ibrahim alipokuwa akifanya kazi kama dreva wa Trekta hiyo. Abas amesema Makonda amepatwa na mkasa huo wa aina yake jana saa 4 asubuhi wakati akitumia compressor mali ya John Tingwa, mkazi wa Kagongwa ambaye pia alikuwepo katika tukio hilo. Habari zaidi zinadai kuwa Tingwa ilijaza upepo bila kuangalia kama tairi imejaa na ndipo ilipopasuka kwa kishindo kikubwa na kumrusha marehemu umbali wa Mita 12 kutoka katika eneo la compressor hiyo na kupoteza fahamu. Hata hivyo wananchi wa eneo hilo walijitahidi kumkimbiza Makonda katika hospital ya wilaya ya Kahama lakini alifariki dunia kabla hajafika katika Hospital hiyo. Kwa upande wake Tingwa ameumia katika mkono wa kushoto na paji la uso na amelazwa katika Hosptal ya wilaya ya Kahama. Jeshi la polisi wilayani Kahama limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wamiliki wa compressor kuwa makini wanapojaza tairi za vyombo mbalimbali vya moto ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima.
Powered by Blogger.