Askari kanzu akitanua njia wakati Mhando (mwenye shati jeupe) akipelekwa kizimbani. Waliounganishwa kwenye kesi hiyo nao wakishuka kizimbani chini ya ulinzi mkali. Mke wa Mhando (kushoto) na mwenzake wakirudishwa mahabusu. MKURUGENZI wa zamani wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) William Geofrey Mhando na mamsap wake, Eva Stephem Mhando, na maofisa wengine watatu wa shirika hilo, France Lucas Mcharange, Sophia Athanas Misidai na Naftali Luhwano Kisinga, leo wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuiingizia serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 884,550,000. Katika kesi hiyo iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Leonard Swai, mbele ya Hakimu Frank Mushi, wakili huyo alisema Mhando akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco anatuhumiwa kumpa tenda mamsap wake ya kusambaza vifaa vya stationery vyenye thamani ya shilingi milioni 884,550,000/ kwa shirika hilo kinyume na taratibu.