TAZAMA PICHA- HII NDIYO SEHEMU AMBAYO MAREHEMU RACHEL HAULE WA BONGO MOVIE NA MWANAYE WATAPUMZIKA DAIMA MILELE
RECHO:
Hapa ndipo atakapo anza siku yake ya kwanza leo kwenye makazi yake
mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi la mtoto wake aliyefariki muda
mfupi baada ya kumzaa katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es
salaam!
RECHO: KUZALIWA 1988 KUFARIKI: 2014. UMRI:miaka 26
Mwili
wa marehemu Recho aliyekuwa msanii wa bongo muvi na mwili wa mtoto wake
kwa sasa unatolewa katika hospitali ya taifa muhimbili na kupelekwa
nyumbani kwao Sinza, na baadaye viwanja vya leaders club kwa ajili ya
kuagwa.
Kwa
mujibu wa mwanahabari Zamaradi Mketema ni kuwa miili hiyo ya marehemu
(Recho na mwanaye itaagwa na ndugu wa karibu kwa dakika chache nyumbani
kwao Sinza na kwenda viwanja vya leaders.
Tukio
hilo limeleta simanzi kwa ndugu jamaa na marafiki na vilio ndiyo
vimetawala kwa wasanii wa bongo muvi waliofika hospitali ya Muhimbili
na kuchukua marehemu.