Wajumbe wa Baraza wawakilishi kutoka CCM katika ziara ya kichama
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Mjumbe wa Kamati Kuu
ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema uamuzi
uliochukuliwa na Vijana wa CCM wa Kijiji cha Kidoti Wilaya ya Kaskazini
“A” Mkoa wa Kaskazini Unguja wa kujiunga na darasa la Itikadi ndio njia
ya msingi itakayowapa fursa Vijana hao kuielewa vyema historia ya Taifa
hili pamoja na Chama chao.
Alisema ipo mikakati
ya makusudi na ya muda mrefu iliyoandaliwa na watu wakiwemo baadhi ya
wanasiasa ya kujaribu kuupotosha ukweli halisi wa Historia ya Taifa hasa
Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyolenga kuwakomboa wakwezi na
wakulima wa Visiwa vya Zanzibar.
Balozi Seif alieleza
hayo wakati akisalimiana na Vijana wa Darasa la Itikadi wa Kijiji cha
kidoti akiwa pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama Tawala
cha CCM walioamua kufanya ziara maalum ya Chama ndani ya mkoa wa
Kaskazini unguja kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2010.