|
‘Hongera sana mheshimiwa kweli umeanza kwa mfano “ |
|
Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala kulia akimpongeza diwani wa kata ya Nzihi kwa kazi nzuri |
|
Wananchi wa Ilala Simba wakimsikiliza mbunge Mgimwa |
|
Uongozi wa kijiji cha Ilala Simba ukimkabidhi mbunge Mgimwa risala yao |
|
Mbunge Mgimwa akikabidhi mipira kijiji cha Ilala Simba leo |
|
Sehemu ya saruji iliyotolewa leo na mbunge Mgimwa |
|
Mbunge
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Nyamihuu katika ziara yake ya kuwashukuru na kupokea changamoto
mbali mbali |
|
Mmoja kati ya wazee walemavu kijiji cha Nyamihuu kalenga akimwomba mbunge Mgimwa msaada wa baiskeli ya walemavu |
|
Kiongozi wa serikali ya kijiji cha Nyamihuu akipokea mipira kwa ajili ya kuendeleza michezo kwa vijana |
|
Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge Mgimwa kwa uchapa kazi wake |
|
Bw Kiswaga akimpongeza mbunge Mgimwa kwa kuonyesha usikivu mkubwa kwa wananchi |
|
MBUNGE wa jimbo la Kalenga
mkoani Iringa Godfrey Mgimwa ameanza kutimiza ahadi zake kwa
wananchi wa jimbo la kalenga kwa kukabidhi mifuko zaidi ya 150 ya
saruji katika kijiji cha Magubike na kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi
yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.5
Saruji hiyo mifuko 100 kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la utawala shule ya sekondari
Dimitrios katika kijiji cha Magubike na mifuko 50 kwa ajili ya shule
ya sekondari Kidamali.
Mgimwa alisema kuwa lengo la
kutimiza ahadi yake hiyo ni kama njia ya kuwashukuru wana Kalenga
kwa kumchagua katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni pia
kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa mbunge aliyefariki
marehemu Dr Wiliam Mgimwa.
Alisema ataendelea kutimiza
ahadi binafsi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa kulingana na uwezo
wake na zile za kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha
anaikumbusha serikali ya CCM ili kutimiza ahadi hizo kwa wakati.
“Ndugu zangu wananchi mbali
ya kuwa ubunge wangu ni wa mwaka mmoja ila tayari mimeanza
kutimiza ahadi bila ya kuchelewa na ninawahakikishieni sita
waangusha nitaendelea kufanya hivyo zaidi mniombee uzima”
Alitaja maeneo ambayo tayari
amekabidhi ahadi zilizotolewa na mbunge aliyefariki kuwa ni pamoja
na Kiwere shule ya msingi mifuko 80 ya saruji,shule ya msingi wangama
bati 100 na saruji mifuko 50,shule ya msingi Negabii bati 100 ,shule ya
msingi Mibikimitali bati 50 ,Kijiji cha Isupilo bati 50 na saruji
mifuko 50 na maeneo mingine mengi.
Pia amekabidhi kiasi cha Tsh
500,000 kwa ajili ya kuchangia kuwezesha kusajili timu ya kata ya
Nzihi na nyingine kwa ajili ya ukarabati wa soko