Eliud (kushoto), akiwa na pacha wake, Elikana -- Daktari aliyewapokea watoto pacha waliokuwa wameungana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwapeleka India kufanyiwa upasuaji, Zaituni Bokhary anatarajia kuwasili nchini leo akitokea masomoni Misri na kwenda Mbeya kuwajulia hali watoto hao. Pacha hao, Elikana na Eliud walizaliwa Februari 20 mwaka jana katika Hospitali ya Wilaya ya Uyole kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na baadaye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuzaliwa wakiwa wameungana kiunoni.