MBUNGE wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya (CCM), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa zamani, jana alijikuta katika wakati mgumu wa kuumbuliwa na mbunge mwenzake wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wakati wawili hao wakibishania uuzwaji tata wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).Hatua hiyo ilijitokeza wakati Mtemvu akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na kuungana na wabunge wenzake kadhaa waliotangulia kuchangia, akidai UDA imeuzwa kifisadi bila wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam kushirikishwa. Wakati Mtemvuakiendelea kujenga hoja yake, Prof. Kapuya aliomba kumpa taarifa, akimwelezakuwa mbunge kujishughulisha na uwekezaji si dhambi na kwamba UDA imeuzwakihalali wala hakuna ufisadi kama inavyodaiwa, isipokuwa mbunge huyo anatumikakuwashawishi wabunge kupinga suala hilo. Baada ya Prof. Kapuya kuketi,