MAAJABU YA HUYU YATIMA, AOTA NYAMA YA AJABU ANA UMRI WA MIAKA 16 ..... KILA ANAYEMLEA HUFARIKI DUNIA
Kwa
kweli duniani kuna mateso, lakini ya mtoto huyu yatima ni makali na
maisha yake yapo hatarini kama hatawahi kupata matibabu. Fuatilia mkasa
wake hapa chini ambao naamini utakuhuzunisha.
Kijana Twaha Sultan (16)
ambaye ni yatima mkazi wa Kipawa Karakata, Wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam akisimulia mkasa wake alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu
zangu, kufuatia maradhi ya ajabu yanayonisumbua sina raha ya maisha,
niheri ningewafuata wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki
nikapumzike.“Nimekuwa mtu wa maumivu wakati wote, kulala na kula kwangu
ni shida tupu mbaya zaidi ndugu ninaoishi nao hawana uwezo.
“Naamini
kama wangekuwa na uwezo huenda ningekuwa nimepona maradhi haya
yaliyoanza kama utani baada ya kunipeleka katika hospitali kubwa na
kupatiwa tiba ya uhakika, kwa kweli nateseka jamani!
“Naumia zaidi ninapowaona
vijana wa umri wangu wakiwa wanasoma na wenye furaha, wakati mimi
nateswa na haya maradhi ambapo nisipopata tiba hatima yangu itakuwa
kifo.
“Kabla ya kuanza kuugua, nilikuwa naishi na wazazi wangu huko Majengo, mkoani Tanga, bahati mbaya mwaka 2000 walitengana.SOMA ZAIDI>>>