AAGA ANAKWENDA MAREKANI LAKINI AKUTWA KAJINYONGA SHAMBANI
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar
es Salaam, Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba,
mwili wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la Abdalah Mshindo jirani na
eneo alilokuwa anaishi.
“Mwili wake ulikutwa ukining’inia baada
ya kujinyonga kwa upande wa kanga alioufunga kwenye tawi la mti wa
mjohoro saa 12 alfajiri juzi,” alisema Kamishna Kova.
Alifafanua kuwa, Julai 27 mwaka huu saa 6
mchana Irene alifika kwenye duka la Oliver Laurent, huku akiwa na pombe
aina ya viroba na dawa nyingi za aina ya mifupein.
“Akiwa dukani hapo, imeelezwa alimwambia
Oliver kuwa anatarajia atasafiri kwenda Marekani kisha akaondoka na
kuingia chumbani kwake, kabla ya mwili wake kukutwa ukining’inia kwenye
mti,” alisema Kamishna Kova.
Uchunguzi wa awali uliofanywa kwenye
chumba chake, uligundua kuwapo vifuko vya pombe aina ya viroba na
hakukuwa na ujumbe wowote kuhusiana na sababu za kujiua kwake.
Katika tukio lingine, dereva wa gari
lenye namba T422 AXV, Toyota Rav 4 ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja, amekufa baada ya gari lake kumshinda na kugonga
mti wa mnazi.
Kamishna Kova alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 4 asubuhi, Barabara ya Kimweli Masaki.