KALI YA MWAKA: MKE AMFUMANIA MUMEWE AKIFANYA MAPENZI NA MBWA WAO, ADAI MBWA HUYO ANA MIMBA YA MUMEWE!!!!!
Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis (pichani), mkazi wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es Salaam amemlalamikia mumewe aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba ametembea na mbwa wao mweusi hadi kumpa mimba.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
“Nililigundua hilo wiki mbili
zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala, nikamsikia mbwa
mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia ili kujua
sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana kumwona mume
wangu yuko naye anafanya mapenzi.
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo.
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia,
nikaamka. Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika
tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza
akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.”
Akaendelea: “Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni
majike na tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja
kwani mara nyingi tunawafungia kwenye banda lao.
“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi (pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.”
Mwanamke huyo alisema kutokana
na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua kuwaeleza majirani ambao nao
walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa eneo hilo.
Akizungumza na Uwazi,
Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka Nyamaishwa alikiri
kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo akamshauri kuyapeleka
kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Habari zaidi zinawekwa
wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke huyo anachelewa kwenda
polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo walitoa taarifa katika
Dawati la Jinsia.
Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na
walalamikaji hao hadi nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na
kuwaamuru wanandoa hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila
kukosa jana Jumatatu saa 3 kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
Uwazi lilimuuliza swali moja
mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na kutoka nje usiku bila
kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani hakuonyesha kushangaa
kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na
hawa majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela
maisha, halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa
yangu kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
Uwazi
lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo
lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila kama huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni
kweli basi yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.”