WAZIRI CHIKAWE ATUA KIGOMA, AKUTANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya (kushoto)
akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe katika
ofisi za Mkoa huo zilizopo mjini Kigoma wakati Waziri Chikawe na maafisa
wake walipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo. Waziri Chikawe
alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo ambapo
walijadiliana masuala mbalimbali ya usalama katika wilaya zote za mkoa
huo. Waziri Chikawe katika ziara yake hiyo, pia anatarajiwa kutembelea
Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya akizungumza
katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Ofisi
yake. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
ambaye pia alishiriki katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili masuala
mbalimbali ya usalama mkoani Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake
waliwasili mkoani hum leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe
licha ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo pia
anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kikao kilichoitishwa kwa ajili yake,
na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Katika
kikao hicho kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa
Kigoma, Waziri na Kamati hiyo walijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi
na Usalama. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo
kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati
hiyo ya mkoa, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo
mkoani humo.Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa
Kigoma. Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu,
Issa Machibya. Waziri Chikawe pamoja na kamati hiyo walifanya kikao
kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma,
wakijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama ndani ya mkoa huo.
Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo kwa ajili ya
ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati hiyo, pia
anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.