AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI NA KUTOLEWA UTUMBO NJE BAADA YA KUTOA MSAADA
Wauaji hao pia walimchoma bibi huyo kisu sehemu ya moyo, mbavu na mkono wa kulia na kutokomea kusikojulikana.
Mtoto wa bibi huyo, Francis Paulo, alisema wauaji hao ambao walikuwa
wawili, walifika nyumbani kwao Ijumaa iliyopita saa 12 jioni
wakilalamikia kuumwa tumbo na kuomba msaada wa kuchemshiwa maji ili
wachanganye na dawa waliyokuwa nayo kujitibu.
Paulo alisema mama yake aliwachemshia maji na kuwapa ili waweze
kutengeneza dawa yao na baada ya kunywa walipumzika wakisubiri wapate
nafuu.
“Baadaye giza lilipoingia baba yangu mzee Paulo Nshimbi (83) alikuja
nyumbani kwangu kukamua maziwa kwa vile sikuwepo na ndama walihitaji
kupewa maziwa,” alisema Paulo.
Anasimulia kuwa kitendo cha mzee wake kuwaaga wageni kilitoa mwanya wa kumuua mama yake.
“Hata hivyo muda mfupi kabla hajakata roho mzee alirejea na kumkuta mama
anahangaika, utumbo ukiwa umetoka nje, amepoteza damu nyingi na
kumtajia jina...."fulani amenichoma kisu amekuja kuniua”, alinukuu
maneno aliyosema mama yake huku akitaja jina la muuaji (jina
linahifadhiwa).
Aliongeza kuwa muuaji alitumia mbinu ya kukodi wageni hao alioshirikiana
nao kumuangamiza mama yake kwa vile alifahamu ratiba ya siku hiyo.
Paulo alisema siku ya mauaji yeye na shemeji yake anayeishi na wazazi
wake, alikwenda kijiji cha jirani cha Bugarama kumsalimia mkwe wao
aliyekuwa mgonjwa.
Alisema walitoa taarifa kituo cha polisi Bugarama na watuhumiwa wandugu
Andrea na Robert Mabala wamekamatwa lakini mhusika ambaye ni
mwanafamilia aliyetajwa na mama yao wakati anakata roho hajaonekana.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanya, Musa Athumani Taibu,
alithibitisha kuwapo kwa mauaji hayo na kueleza kuwa mtuhumiwa ametoroka
na polisi inaendelea na msako.