TAMASHA LA UPENDO KWA LAKARIBIA SASA MASHABIKI NA WAPENZI WA NYIMBO ZA INJILI WAHESABU SIKU.
Lile tamasha kubwa la Injili lilokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na awakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake sasa limekaribia kufanyika ambapo mashabiki na wapenzi wa nyimbo za Injili wanahesabu siku tu kufikia tamasha lenyewe.
Tamasha hilo lijulikanao kama UEPNDO KWA MAMA ambalo linawashirikisha wasanii maarufu wa nyimbo za injili kutoka Tanazania na nje ya nchi limekuwa likivuta hisia kali sana kwa mashabiki na wakazi wengi wa jiji la Arusha pamoja na viunga vyake jambo ambalo linasababisha Tamasha hilo kuwa na muonekano wa Tofauti na matamasha mengine.
Sababu kuu ya kuwa na sura ama mtazamo tofauti ni kutokana na wasanii hao huwa na mashabiki na wapenzi wengi wa nyimbo hizo jambo ambalo linasababisha kujitokeza kwa wingi kuja kuwashuhudia wasanii hao ambao wamevuta hisia za watu wengi kuto hata nje ya nchi.
Wasania hao ambao watakuwepo katika tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa ni pamoja na UPENDO NKONE,MARTHA MWAIPAJA,CHRISTINA SHUSHO,SARAH K,ENG CARLOS MKUNDI,MASSA BARAKA pamoja na wasanii wengi kutoka ndani ya mkoa wa Arusha pamoja na Mikoa jiranib ambao pia watapewa nafasi ya kuhudumu siku hiyo ya Tarehe 2 Nov2014 katika Uwanja wa Shekh Amri Abed Jiji Arusha.
Lengo kuu la tamasha hilo ni kuonyesha UPENDO KWA WAKINA MAMAM pamoja na kuwasaidia ama kuwawezesha kiuchumi wamama wote wenye mahitajio ya kufanya hivyo,Tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Mkundi Production kutoka Jijini Arusha.