Header Ads

BAYERN YAItandika DORTMUND 3-0

bayern2 b346c
Bayern Munich (HM)
bayern eb2d8
MSHAMBULIAJI Mario Goetze ameifunga klabu yake ya zamani, Borussia Dortmund ikilala 3-0 mbele ya wapinzani Bayern Munich katika mechi kali ya timu mbili zinazofukuzana kuwania ubingwa usiku wa jana.
Goetze alifunga dakika ya 66, dakika 10 tangu aingie kutokea benchi, The Bavarians wakishinda mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Dortmund tangu 2010.
Arjen Robben alifunga bao la pili zikiwa zimesalia dakika tano na Thomas Mueller akahitimisha karamu ya mabao ya Bayern. Chanzo: Sportmail
Powered by Blogger.