Header Ads

MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI KANDA YA KASKAZINI YAONGEZEKA

.
Mwakilishi kutoka katika shirika la kupambana na maambukizi ya UKIMWI Mkoa wa Arusha Bi Blandina Nkindi akiwasilisha Takwimwi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Bw Gaudens Lymo kulia  akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa chama cha watu wanoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi (TUPO)Bw Emanuel





Imeelezwa kuwa kanda ya kaskazini hususani Mkoa wa Arusha maambukizi ya virusi vya UKIMWI yameongezeka toauti na miaka iliyo pita kwakufikia  3.2%kutokana na Mila na desturi pamoja na Arusha kuwa kituo cha utalii.
Takwimu hiyo imetolewa na mwakilishi wa shirika la kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka mkao Bi Blandina Nkidi katika semina iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa Habari za michezo Mkoa wa Arusha TASWA Ili kuuwezesha mfuko wa TUPO cha watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
Amesema hali ya ukimwi kati ya mwaka 2003-2004 ilikuwa asilimia 5.4 na kushuka kutokana na juhudi mbalimbali za kupambana na ugonjwa huo kati ya mwaka 2007-2008maambukizi yalikuwa asilimia 1.6 ambapo ilikuwa ni hatua nzuri ya kupambana na maambukizi mapya.
Amesema tatizo kubwa lililochangi maambukuzi hayo kupanda nikutokana na mila na desturi,ulevi wa kupindukia,mwingiliano wa wageni mbalimbali watu kutokuwa na hofu ya Mungu kwakuwa wengi wao huufananisha ugonjwa huo kama malaria pamoja na ushirikishwaji wa wakina baba katika mpango wa uzazi salama.
Pamoja na hayo Mstahiki meya wa Jiji la Arusha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo Bw Gaudens Lymo amesema ongezeko hilo ni tishio kwa Taifa kwani jamii imeshindwa kutambua wajibu wao wa kupambana na maambukizi hayo .
Amesema kuwa vijana wengi ndio wamekuwa katika hatari kubwa ya kupatwa na mabukizi ya virusi vya UKIMWI hivyo kuwataka kuchukua tahadhari  kujiepusha na maambukizi hayo.
Sambamba na hayo mashirika mbalimbali yaliyo husika katika kudhamini semina hiyo yakiwemo PPF,PSI,LAP,TACAIDS Pamoja na Ausha Press Club ambao ndio waandaaji wa semina hiyo wamewataka wanachama wa TTUPO ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kujiunga na mifuko mbalimbali ili kuweza kupata msaada wakati wanapokabliwa na matatizo.
Kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha TUPO Mkoa wa Arusha bw Emanuel amesema licha ya kuwa na mafanikio katika chama hicho zipo changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa Fedha Kuwaela watoto,usafiri,lishe bora pamoja na mambo mengine hivyo kutoa wito kwa Taasis mbalimbali kuonesha ushirikiano.
Katika semina hiyo pia wageni wlioalikwa waliweza kupata fursa ya kufundishwa juu ya virusi vya UKIMWI jinsi mtu anavyoweza kuambukizwa pamoja na jinsi ya kujikinga dhidi ya maambukizi hayo
……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Powered by Blogger.