WAMBURA AKAIMUSHA MIKOBA YA ANGETILE OSIAH TFF
Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Bw.
Boniface Wambura kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Uteuzi huo ni kuanzia
Novemba 2 mwaka huu.
Aidha aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ameagizwa aende likizo ya malipo hadi atakapomaliza mkataba wake.
Kamati
ya Utendaji inaviomba vilabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama
shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Bw. Boniface Wambura katika
utekelezaji wa majukumu yake.
Jamal Malinzi, Rais TFF
Dar es Salaam
Novemba 3, 2013