WANAWAKE WAPEWA KIPAUMBELE CHA UONGOZI JUU YA UUNDWAJI WA KATIBA NDANI YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI (A.J.T.C)
Mchakato unaoendelea
ndani ya chuo cha uaandishi wa habari na utangazaji Arusha juu ya uundwaji wa katiba mpya ya wanachuo umekuwa na mfumo tofauti
baada ya wanawake kuteuliwa na wizara ya sheria na katiba kushika ngazi za
uongozi katika baraza hilo la katiba.
Wanawake hao ambao
wameteuliwa ndani ya baraza hilo ili kusimamia mchakato huo ukiwemo utoaji wa
maoni mpaka kukamilika kwa katiba hiyo wamekuwa wengi kuliko wanaume
walioteuliwa ndani ya baraza hilo jambo ambalo linatoa taswia ya wanawake
kupewa kipaumbele kikubwa.
Katibu wa baraza hilo
bi Emelda Stephano amesema kuwa lazima jamii itambue kuwa wanawake wanuwezo
mkubwa sawa na wanaume katika utendaji wa
kazi na utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika Nyanja za kiongozi.
Licha ya hayo amesema
wanafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha mchakato huo unakamilika kwa kiwango
kilichotarajiwa kwani wanachuo wamekuwa wakiongozwa bila kuwapo kwa katiba
ambayo inawaongoza na kushindwa kutambua
taratibu za chuo.
Nae Mwenyekiti wa
baraza hilo bw Oska Samba amesema wameamua kuteua wanawake wengi
kushika nyadhifa hizo za kiongozi na
wengine kuwa wajumbe ndani ya baraza hilo ili kuwajengea uwezo na uzoefu wa
utendaji kazi katika nafasi za kiongozi
tofauti na ilivyozoeleka.
Amesema kuwa
mabadiliko na kipaumbele cha kuwateua
wanawake hao katika baraza la uundwaji wa katiba imeleta chachu ya utendaji wa
kazi kwakuwa kila mmoja wao anajitahidi kuonyesha uwezo wake wa utendaji wa
kazi na hiyo kufanya zoezi hilo kwanda haraka tofauti na walivyotarajia.
Katika mchakato huo
wanachuo hao wamepewa fursa ya kutoa maoni yao juu yanini kiwepo ndani ya
katiba hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwao pamoja na vizazi vijavyo hasa katika
tasnia kongwe ya Uandishi wa habari hapa nchini hasa kwa kutambua haki zao za
kimsingi katika taaluma yao
Baraza hilo la katiba
ambalo liliteuliwa na waziri wa sheria na katiba bw.Agape Msumari linatarajia
kumaliza kukusanya maoni ya uundwaji wa katiba siku ya jumanne tarahe12Nov2013
ambapo itatoa fursa kwa wizara ya sheria na katiba pamoja na baraza kujadili
maoni hayo.