Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akutana na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia Kujadiliana Kuhusu Masuala ya Gesi Nchini
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongoza kikao
kati yake na Ujumbe kutoka Benki ya
Dunia pamoja na Watendaji wa Wizara. Kikao hicho kimejadiliana kuhusu suala
zima la Gesi nchini na hatua mbalimbali zilizofikiwa hadi sasa.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuzungumzia Masuala ya Gasi nchini. Miongoni mwa Masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuhusu hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa hadi sasa na Serikali kuhusu Sekta hiyo. Aidha, kikao hicho pia kimewashirikisha Watendaji kutoka Wizara hiyo wanaosimamia masuala ya Gesi Asilia na Nishati.
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiongoza
kikao kati yake na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia pamoja na Watendaji wa
Wizara. Kikao hicho kimejadiliana kuhusu suala zima la Gesi nchini na
hatua mbalimbali zilizofikiwa hadi sasa.
Kamishna Msaidizi anayesimamia Masuala ya Gesi Asilia Engineer. Bw. Nobert Kahyoza akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Kamishna
Msaidizi anayesimamia Maendeleo ya Nishati Bw. James Andilile
akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho baina ya Wizara na Ujumbe toka
benki ya Dunia.