CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: AZAM YATUPWA NJE HUKO BEIRA!
LEO
HII, huko Beira, Msumbiji, Azam Fc ikicheza Mechi ya Marudiano ya
Raundi ya Awali ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho, ilifungwa
Bao 2-0 na Ferroviario de Beira na kutupwa nje kwa Jumla ya Bao 2-1.
Wiki iliyopita huko Azam Complex,
Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC iliifunga
Ferroviario de Beira Bao 1-0.
Hapo Jana, Wawakilishi wa Zanzibar
kwenye Michuano hii ya Kombe la Shirikisho, Chuoni, walifungwa 2-1 Mjini
Zanzibar na How Mine ya Zimbabwe na kutolewa kwa Jumla ya Bao 6-1 kwani
Wiki iliyopita huko Zimbabwe walinyukwa Bao 4-0.
Timu nyingine ya Zanzibar inayocheza
Michuano ya Afrika, kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI, ni KMKM ya Zanzibar ambao
Leo huko Visiwani Zanzibar wanarudiana na Dedebit ya Ethiopia huku
wakiwa nyuma kwa Bao 3-0 baada ya kuchapwa Wiki iliyopita huko Ethiopia.
Timu pekee ya Tanzania ambayo
imefanikiwa kusonga kutoka Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI ni
Yanga ambayo Jana hukO Comoro waliibonda Komorozine de Domoni Bao 5-2 na
kuitupa nje kwa Jumla ya Bao 12-2 kwani waliifunga 7-0 Wiki iliyopita
Jijini Dar es Salaam.
Yanga sasa watacheza Raundi ya Kwanza ya
CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Al Ahly ya Misri ambao ndio Mabingwa
Watetezi na Mechi hizi zitachezwa kati ya Februari 28 na Machi 2 na
Marudiano ni kati ya Machi 7 na 9.
Kwenye Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho, Ferroviario de Beira watakutana na ZESCO ya Zambia.