Mh. Lowassa akana umiliki wa kurasa za mitandao ya kijamii
Kumekuwa
na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mh. Edward Lowassa Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mitandao ya
kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.
Zinazoonye kuwa mmiliki wake ni Mh. Edward Lowassa.
Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote hazimilikiwi na Mh. Lowassa.
Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,hazihusiani kwa namna yoyote na Mh. Lowassa.
Hata
hivyo Mh. Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya
ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.
Imetolewa na
Ofisi ya Mh. Edward Ngoyai Lowassa
Mbunge wa Jimbo la Monduli.