SALAAM KWA YANGA MBELE YA MKWASA JUKWAANI!!
SALAAM KWA YANGA MBELE YA MKWASA JUKWAANI!!
MABINGWA
wa AFRIKA, Al-Ahly ya Misri, wametwaa Kombe la CAF SUPER CUP baada ya
kuichapa Klabu ya Tunisia CS Sfaxien Bao 3-2 Uwanja wa Kimataifa wa
Cairo Jijini Cairo, Nchini Misri.
CAF SUPER CUP hushindaniwa kila Mwaka na
Bingwa wa CAF CHAMPIONZ LIGI na Timu inayotwaa CAF Kombe la Shirikisho
na safari hii Al Ahly walicheza kama Bingwa wa CHAMPIONZ LIGI na CS
Sfaxien ndio waliotwaa Kombe la Shirikisho Mwaka Jana.
Wakishangiliwa na Mashabiki wao 30,000,
Al Ahly walitangulia kufunga Bao kupitia Straika Mohamed 'Gedo' Nagy
ambalo lilidumu hadi Haftaimu.
Kipindi cha Pili, Amr Gamal aliipa Al
Ahly Bao la Pili na Fakhreddine Ben Youssef kuifungia CS Sfaxien Bao lao
la kwanza lakini Amr Gamal tena akapiga Bao la 3 kwa Al Ahly.
Nahodha wa CS Sfaxien, Ali Maaloul, alileta mshikemshike kwenye Mechi hii baada ya kufunga Penati na kufanya Gemu iwe 3-2.
Lakini Al Ahly walisimama imara na
kulinda Bao zao na kutwaa SUPER CUP hii ikiwa ni mara ya 6 na ni rekodi
na kuwaacha CS Sfaxien wakishikilia rekodi ya kulikosa Kombe hili mara
tatu.
Ushindi huu ni ahueni kubwa kwa Kocha wa
Al Ahly, Mohamed Youssef, ambae Timu yake imechapwa mara 3 kwenye Ligi
yao na Timu dhaifu.
Miongoni mwa Watazamaji wa Mechi hii ni
Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ambae alipelekwa rasmi
Jijini Cairo kuichunguza Al Ahly ambayo watakutana nayo kwenye Mechi ya
Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ hapo Machi Mosi Jijini Dar es Salaam.