NHC KUNEEMESHA WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI NCHINI
Mfanyakazi wa NHC akiweka nembo ya shirika hilo. |
SHIRIKA
la nyumba la Taifa NHC linatarajia kujenga Nyumba 500 za watu wenye
kipato cha chini zinazotarajiwa kujengwa katika eneo la Mateves jijini Arusha,ikiwa
ni moja ya mkakati wa shirika hilo kuhakikisha kuwa Watanzania hasa
wenye hali duni kiuchumi wanapata makazi bora na ya kisasa kwa gharama
nafuu.
Akizungumza jana jijini Arusha Mkurugenzi wa biashara na Maendeleo wa NHC ,David Shambwe katika kikao cha Wizara ya Ardhi,Nyumba na Makazi ya makazi kilichojumuisha Viongozi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,
alisema kuwa watashirikiana na mabenki ambayo yanatoa mikopo ya muda
mrefu kuanzia miaka 10-15 ili kuwawezesha watu wa hali ya chini kumiliki
nyumba hizo kwa mkopo.
“tutajenga nyumba 5000 mikoa yote ya Tanzania yenye wilaya 150 kwa wastani tutajenga nyumba 50 kila wilaya” alisema Shambwe
Alisema
mpango huo unatarajia kuzinduliwa rasmi April mwaka huu na kutekelezwa
kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itajengwa nyumba 200 mradi
utakaoanza mwezi ujao huku awamu ya pili ikiwa ni nyumba 300 kwa
kushirikisha wawekezaji katika kuteleza mpango huo.
Aidha
ameeleza kuwa nyumba hizo 500 kwa wastani nyumba moja inakadiriwa
kuuzwa kiasi cha shilingi milioni 30 na kuwataka Watanzania watumie
fursa hiyo kujipatia makazi bora na lengo la NHC ni kupanga miji na kuondokana na tatizo la ujenzi holela.
Kwa
upande wake Mshauri wa Masuala ya mipango miji kutoka kampuni ya
Surbana Urban Group ya nchini Singapole ,Anandan Karukaran ameishauri
serikali iweke mipango ya kutawanya shughuli za maendeleo nje ya jiji
ili kupunguza msongamano katikati ya miji.