Header Ads

TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Member of Parliament for Nzega | P. O. Box 415, Nzega. Tabora | Cell: +255782636963

1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA
OFISI YA MBUNGE, JIMBO LA NZEGA
Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (MB), 
Mwenyekiti, Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
KUMB. NA. MP/PR/001/2014                                                                       Tarehe: Feb 14, 2014
TAMKO LANGU KWA UMMA KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA
KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Ndugu wanahabari na waTanzania wenzangu,
Nimekuwa nikilazimika kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanahabari, ndugu, jamaa na marafiki
kuhusiana na namna mchakato wa kuandika katiba mpya ya Taifa letu unavyoenda; wengi wakipenda
kujua nini mtazamo wangu kuhusu mambo mengi, haswa hili la serikali mbili ama tatu kwenye
muungano wetu. Mara nyingi nimekuwa nikikwepa kusema msimamo wangu ni nini kwa sababu niliona
ni vema nikajipa muda wa kutafakari kabla ya kuamua kujenga msimamo yangu. Ila kwa kuwa wakati wa
kwenda Bungeni umefika na mimi nimepata bahati ya kuwa miongoni mwa wajumbe wa Bunge hili la
kihistoria nimeona leo nitoe mtazamo wangu.
Kwanza, nianze kwa kuonesha wasiwasi wangu kama tutaweza kufika salama huko tuendako. Si kwa
sababu za kitabiri kama mnajimu, la, ni kwa sababu za kisayansi, ambazo nitaziweka wazi hapa kama
ifuatavyo:
(i.)          Pamoja na kwamba tume imefanya kazi nzuri ya kukusanya maoni na kuyaweka katika
nyaraka ambayo tutapaswa kuifanyia kazi, napata shida kama walikuwa makini katika
kuendesha zoezi hili. Kivipi, binafsi napata shida na methodology iliyowawezesha kufikia
‘conclusion’ madhubuti kwamba watanzania asilimia 61 walitaka serikali tatu. Kwa sababu
za kisayansi naona tume ya Mhe. Jaji Warioba imepotoka na kwamba kusema hivyo ni
kutaka kulazimisha uhalali wa hoja hii nyeti kwenye dokumenti ya Rasimu ya Katiba
tunayopaswa kuipitisha bila kuwa na msingi wa kitakwimu unaotokana na njia
(methodology) za kisayansi za kukusanya ‘data’ na kutafuta ‘validity’ na ‘generalizability’ ya
taarifa husika.  Nilidhani hili milikuwa na muda wa kutosha kama chama na kama wabunge
kulitizama. Inasikitisha sana kusikia kuwa leo ndio linaonekana. 
        
(ii.)          Kwa jinsi mchakato ulivyo ni ngumu kusema kuwa leo tutaweza kubadili jambo nyeti
kama la ‘Muundo wa Muungano’ kuwa uwe ni wa Serikali mbili, ama moja, wakati
mapendekezo ya Tume, ambayo ‘yanaelezewa’ na Tume kuwa yanatokana na ‘maoni’ ya
wananchi walio wengi, 61% na pili mabaraza ya katiba [cf. Muundo katika mchakato huu ni
Member of Parliament for Nzega | P. O. Box 415, Nzega. Tabora | Cell: +255782636963

2
wa pyramid, kwamba unaanza na maoni ya wengi huku chini kwenye kitako, baadaye
mabaraza ya katiba hapo katikati na mwisho Bunge la Katiba, kabla ya kura ya maoni]. Hivi
inawezekana wapi Bunge Maalum la Katiba, kwa hapa tulipofikia, likafanya mabadiliko
kwenye mambo yanayohusu ‘muundo’ (structure) wa Katiba? Yaani, kwamba inawezekana
vipi wajumbe hawa 640 wabadilishe jambo zito la kimuundo kama hili? Kimantiki haingii
akilini. Uhalali huo unatoka wapi? Lakini pia hapa hatuwezi kuondoa ukweli kwamba
malalamiko na manung’uniko ya baadhi ya watu yana mashiko, kuwa hivi kama hoja ya
Chama Cha Mapinduzi ilikuwa ni kuilinda ‘status quo’ ya muungano wa serikali mbili na
kama walifanya kazi ya kuwaelimisha wanaCCM nchini, na wanaCCM walikuwa wengi zaidi
kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya [walishinda kwa zaidi ya asilimia 65, inatokeaje
asilimia 61 watake muungano wa serikali 3?]. Maana yake ni kuwa hata wanachama wa ccm
ngazi ya wilaya walichagua serikali tatu. Au inawezekana kuwa walitumwa kutoe hiyo elimu
/maelekezo hawakuwa na nguvu (mbinu na weledi) ya ushawishi. Lakini pia ni somo kuwa
sio sawa kuamini kuwa wanachama wa ccm ngazi ya wilaya hawawezi kutafakari na
kuchagua, eti wao ni wa kupewa elimu na kufuata tu.   

Nini tafsiri ya haya yote? Kwamba ukisema unabadili leo muundo wa Muungano ukaleta
wazo tofauti na lile linalotokana na mapendekezo ya tume, kama yanavyosomeka kwenye
Rasimu (sura ya 6), mfano ukasema, ziwe serikali mbili tu badala ya tatu zinazopendekezwa,
maana yake unaongelea kuanza upya kutengeneza vifungu vipya vya ‘kimuundo’ vya serikali
za mitaa, wawakilishi wa wananchi, mambo ya wakuu wa mikoa ama majimbo(provinces) –
jambo ambalo litakuwa cumbersome! Vurugu mechi bila uwepo wa rasimu! Swali la kujiuliza
hapa ni kwamba – hivi tume hawakuliona hili? Pengine wangeweka chaguzi (option)
pembeni, maana maoni yote haya wanayo, ila kwa sababu ya muundo wa Muungano
‘waliouchagua’ hawakupenda kuelezea mambo binafsi ya serikali hizi ‘mbili’ za ‘iliyokuwa
Tanganyika’ na Zanzibar kwa madai kwamba jukumu lao ni kuandaa rasimu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachoonekana hapa ni kwamba walikwishaamua
kuwa ziwepo serikali tatu kwa madai kuwa ndiyo maoni ya wananchi na kwa kuzingatia
msingi wa hoja kwamba Bunge la Katiba haliwezi kuwa na uhalali wa kubadili mambo ya
msingi ya kimuundo wa katiba, kama hili la Muundo wa Muungano, bali ‘kuboresha’ tu yale
yaliyomo. Mtu makini atahoji kuwa ni kwa nini wamekwepa kuzungumzia ukweli kwamba
‘Tanganyika’ hayupo? Na nini itakuwa hatma ya Katiba yake? Na ni lini wabia hawa wa
Muungano walikaa wakakubaliana washirikiane kwenye mambo yapi kwenye huo
muungano wa Shirikisho? Hili la tanzanyika kwa ujumla wake halikuwepo katika ToR na pia
unajenga hoja kwa kuhisi tu hasa unaposema alikuwa “wameshaamua”.  

Sasa wabunge wa Bunge maalum la katiba tukiukataa huu muundo wa serikali tatu nini
kitatokea? Maana yake sehemu kubwa ya rasimu hii italazimika kubadilishwa. Hakika ! Lakini
kama ulivyosema wewe mwenyewe watapata wapi hayo mamlaka?

       Jambo lingine ambalo litatusumbua ni kuwa, vipi kama wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba tukiamua tujenge msimamo kwenye hoja ya Serikali Moja itakuwaje? Maswali mengi
yataibuka bila kupata majibu hapa, kuwa ni nani atakuwa ‘Mpatanishi’ kwa niaba ya
Tanganyika (ama Tanzania bara)? Maana Zanzibar yupo na ana uhai wake kamili, Tanganyika
yuko wapi hapa? Hakika ! Lakini kama ulivyosema wewe mwenyewe watapata wapi hayo
mamlaka? Na kama mkiamua hivyo mnatakiwa muwe na majibu ya hayo maswali na pia
hamtahitaji siku 70 huko! 
Member of Parliament for Nzega | P. O. Box 415, Nzega. Tabora | Cell: +255782636963

3
(iii.)  

Mhe. Jaji Joseph Warioba na wenzake wanapaswa wajibu maswali haya:

1.  Ni njia (methodology) ipi ya kisayansi na kitakwimu walitumia kufikia ‘conclusion’ hiyo
madhubuti kabisa kuwa 61% ya watanzania walitaka Muundo wa Serikali Tatu? Watueleze
watanzania sample size, sampling technique, sampling frame na namna walivyowafikia na
kuwahoji watu hao. Hili jibu lake wanalo na hata wewe unajua watalijibu vizuri sana. Ingawa
aliewapatia ToR anatakiwa kujua zaidi, vilevile ninashangaa ilikuwaje mkakubali rasimu ya
kwanza bila kujua methodology nk ? 

2.  Watueleze ni nani aliyewatuma kwenda kubadilisha Muundo wa Muungano?  Hapa nadhan
kaka umesahau kuwa hawa jamaa walitumwa kukusanya maoni kuhusu Muungano, kimsingi
unawezaje kuzungumzia muungano bila kuzungumzia muundo, na kama ukiuzungumzia,
unawezaje kukwepa watu kuutolea maoni? 

3.  Ni nani sasa atakuwa na mamlaka ya kuandika Katiba ya Serikali ya Tanganyika (ama
Tanzania Bara – ambaye aliishakufa?), kama tukiamua kwenye Bunge la Katiba kupitisha
Rasimu hii yenye Muundo wa Muungano wa Serikali tatu? Tunaanzia wapi kumfufua
Tanganyika? 
Hili ni swali zuri sana kaka, ila ninashangaa kwa nini wizara na mkuuw a nchi hajajibu mpaka
sasa. Hili ni swali ambalo ninyi wabunge mlitakiwa kuliona kabla na kuhoji, ila kwa sababu
mnazozijua ninyi hamkuhoji na leo unatoa tamko tu badala ya kuhoji wahusika…Kimsingi ukiwa
mwenyekiti wa kamati ya TAMISEMI na ukijua kuwa ninyi ndio mhimili wa serikali na katiba ya
Tanganyika na mpaka leo mnaona sawa tu kuendelea na mchakato bila majibu ya “iko wapi
serikali ya mitaa na vijiji?”  

Maoni yangu: Mtu yeyote mpenda demokrasia ataona wazi kwamba kuna utata uliogubikwa na
ukungu wa presha za kisiasa za kuona zoezi hili linakamilika. Utata wa uhalali wa Bunge la Katiba
kubadili hoja za msingi kwenye rasimu ni jambo zito, na mashaka kwamba pengine Jaji Joseph
Warioba na wenzake walikuwa na ajenda yao ya siku nyingi ya kuleta serikali tatu kinyume na
matakwa ya Chama Tawala, CCM, ni jambo zito zaidi. Hivyo, kuondoa mamlaka na madaraka ya
wananchi (kama kweli yapo kama inavyosema tume) kwenye jambo zito la kimsingi kama
Muundo wa Muungano ni jambo linalotishia usalama wa mchakato na ni jambo lisilokubalika
kwa kuwa linaondoa haki, wajibu, mamlaka na madaraka ya wananchi kufanya maamuzi kuhusu
katiba yao (an act of popular sovereignity). Mkanganyiko huu unatia mashaka zaidi ya kuleta
mwangaza wa mabadiliko ya kutokea kwa maridhiano. Jaji Warioba na wenzake walilijua hili na
wameleta ‘chaos na frustration’ kwa maksudi kwa kujificha chini ya kivuli cha ‘uhalali’ wa Bunge
la katiba HAO WENZAKE NI KINA NANI AMBAO HATA WAKO TAYARI KUWA KINYUME NA CCM ?
HII INATISHA KIDOGO (yaani ‘legitimacy of rule or of law is based on the consent of the
governed’) na nadharia pana ya demokrasia yenye msingi kwenye kanuni za ‘popular
sovereignity’ wakijua kabisa wabunge tutashindana, tutatofautiana!

Mimi nina maoni kwamba, ili mchakato uishe salama, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete aingilie kati, atumie mamlaka yake kusitisha mchakato huu mpaka
itakapoundwa tume nyingine ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu suala la Muundo wa
Member of Parliament for Nzega | P. O. Box 415, Nzega. Tabora | Cell: +255782636963

4
Muungano na kisha ipigwe kura maalum ya maoni kuhusiana na jambo hili ili watanzania
washiriki kikamilifu na waamue na siyo kufanya maamuzi ya kubadilisha Muundo wa Muungano
bila kutupa fursa ya kujadiliana na kushiriki kufanya uamuzi kuhusu jambo hili. Ni jambo lisilo na
busara hata kidogo kwenda kujadili Rasimu ya Katiba bila kuwa na suluhu inayokubalika kuhusu
Muundo wa Muungano wetu. HAPA KAKA UMETUMIA MANENO MAKALI KIDOGO, YAANI HUONI
BUSARA ? ANYWAY MIMI NINADHANI NDIO MAANA YA KWENDA KUJADILI UNLESS UNA
WASIWASI NA UWEZO WA HAO WANAOTAKIWA KUJADILI…. ILA KAMA UNATAKA KUPATA
“SULULU INAYOKUBALIKA” BILA KUJADILI SIDHANI KAMA UNAWEZA KUIPATA.   

Kama kuna presha ya muda wetu wa miaka mitano kuisha kuna dirisha la kutokea; tusogeze
mbele muda wa uhai wa Uongozi wa awamu hii ama turudi nyuma tufanye mabadiliko ya
sehemu za katiba zinazohusiana na Tume ya Uchaguzi tu. Hatuna namna ya kukwepa moja kati
ya mambo haya kwa sababu hata tukifanikiwa kufunika kombe mwanaharamu apite, tukapitisha
Katiba hii, INAONESHA KUWA HAKA KATABIA KAPO NA HUENDA KAMELETELEZA MKANGANYIKO
AMBAO UNAUONA LEO, LAITI MSINGEKUWA MNAFUNIKA KOMBE LEO USINGEPATA
SHIDA….bado tutahitaji kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria mbalimbali nay a kitaasisi
kutokana na Katiba mpya itakayokuwa imepatikana, zoezi ambalo kwa kila namna litahitaji
muda wa kutosha na sioni kama upo! Demokrasia ni gharama na haikwepeki! 

Maswali ni mengi zaidi ya Majibu. Wasiwasi ni mwingi kuliko uhakika. Tutafika salama kwenye
kupata Katiba hii kweli? Ni bora tukawie kuliko kuvurunda. Tusikimbie kwa kasi bila kutazama
tuendako, tutambae lakini macho njiani na mbele tunakoelekea. 

Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Nzega.

          HK (Nimesaini)
Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB. 
Powered by Blogger.