UCL: JUMANNE-OLYMPIACOS v MAN UNITED, JUMATANO-GALATASARAY v CHELSEA!
>>UNITED, CHELSEA KUISAFISHA ENGLAND BAADA CITY, ARSENAL KUCHAPWA MBILI MBILI NA NYEKUNDU JUU??
>>REAL NAO UGENINI GERMANY NA SCHALKE!
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
+++++++++++++++++++++++++++++++++
BAADA
WIKI ILIYOPITA kushuhudia Mechi 4 za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu
16 za UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Mashindano hayo yanaendelea tena
Jumanne na Jumatano Wiki hii kwa Mechi nyingine za kwanza 4 za Raundi
hiyo ambapo Timu mbili za England, Mabingwa Manchester United na
Chelsea, zitakuwa Ugenini kuanza kampeni zao.
Wiki iliyopita, Timu nyingine mbili za
England zilianza vibaya kwa zote kufungwa Mechi zao za Nyumbani wakati
Man City walipochapwa kwao Etihad 2-0 na Barcelona na kumaliza Mechi
wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao, Martin Demichellis, kutolewa nje kwa
Kadi Nyekundu.
Hali kama hiyo iliwakuta Arsenal
walipopigwa 2-0 Uwanjani kwao Emirates na Bayern Munich na kumaliza
Mechi hiyo Mtu 10 baada Kipa wao Wojciech Szczesny kutolewa nje kwa Kadi
Nyekundu.
Wiki hii, Man United watakuwa huko
Ugiriki kucheza na Olympiacos na Meneja wao, David Moyes, licha ya
kukiri ni Mechi ngumu, amesema wao wamepania ushindi wa huko huko
Ugenini.
Nao Chelsea watakwenda huko Uturuki
kupambana na Klabu Kigogo ya huko, Galatasaray Spor Kulübü, ambayo
Straika wake ni Didier Drogba, Gwiji wa zamani wa Chelsea, ambae Mechi
yake ya mwisho na Klabu hiyo ya Engand ni kuifungia Penati ya mwisho
katika Mikwaju ya Penati 5 walipoitoa Bayern Munich kwenye Fainali ya
UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Munich Mwaka 2012 na kutwaa Ubingwa.
Lakini Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, amesema urafiki na Drogba utakuwa haupo kwa Dakika 90.
UEFA CHAMPIONZ LIG
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MATOKEO:
Jumanne Februari 18
Manchester City 0 FC Barcelona 2
Bayer 04 Leverkusen 0 Paris Saint-Germain 4
Jumatano Februari 19
AC Milan 0 Atletico de Madrid 1
Arsenal FC 0 Bayern Munich 2
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP