YESU FEKI ANAVYOTIKISA DUNIA, ANATAKA KUJA DAR ES SALAAM
SHETANI
bado anazidi kuwasakama Wakristo duniani. Hii ni baada ya mkazi wa
Kijiji cha Alvaro Thesiss, Santa Catarina nchini Brazil, Mtume Inri
Cristo (66) mwanzilishi wa Kanisa la Waraka Mweusi (Suprema Ordem
Universal da SantÃssima Trindade ‘Soust’), miaka 35 iliyopita
kujitangaza kuwa yeye ni Yesu Kristo amerudi kuja kuwaokoa wanadamu
baada ya kusubiriwa kwa miaka mingi.
Cristo
kwa sasa anaitikisa dunia kwa kuwahubiria maelfu ya watu wa madhehebu
ya Kikristo sehemu mbalimbali duniani huku akijiita Yesu Kristo wa
Nazareti.
MAHUBIRI YAKE YATIKISA
Mei, 2013, Cristo alitua katika Jiji la Sao Paulo nchini humo na kuwaombea Wakristo, wakiwemo makahaba. Alipokelewa kwa heshima zote huku akijitangaza kuwa hakuna atayekuja duniani kuwakomboa wanadamu zaidi yake.

Alihubiri kuwa kwa kila kiumbe mwenye matarajio ya kuingia kwenye ufalme wa mbinguni yeye ndiye njia ya kweli na uzima.
YESU FEKI AKUTANA NA MAGUMU
Septemba, 2013, mzee huyo alitua kwenye Jiji la Rio de Jeneiro kwa lengo hilohilo lakini alijikuta akishambuliwa vikali huku Wakristo wa jiji hilo wakimtupia lawama kuwa ni mhubiri feki aliyevaa ngozi ya kondoo kujipatia kipato kinyume na utaratibu wa makanisa mengine ya Kikristo nchini Brazil.

AITWA MHUBIRI PUNDA
Akiwa katika harakati zake za kuwavuta waumini wa makanisa ya Kikristo katika Jiji ya Sao Paulo wakati wa Sikukuu ya Krismasi, mwaka jana, mhubiri huyo feki alishambuliwa tena na waumini wa eneo hilo ambao walikusanyika kwenye mkesha wa sikukuu hiyo.

Baadhi
ya waumini walimzomea kwa mahubiri yake huku wakisema hayana tofauti na
punda aliyebebeshwa mzigo mzito na kushindwa kuutua.
Hata
hivyo, Yesu feki huyo aliwajibu waumini hao kwamba hawajui walitendalo
kwani yeye ndiye Yesu wa kweli aliyetumwa na Mungu kuja duniani kuwaokoa
wanadamu.
“Mimi
sijali maneno yao, wameniita punda, eti mahubiri yangu hayana tofauti
na punda aliyebebeshwa mzigo mzito hivyo hawezi kujinasua siku zote
ataishia kutapatapa, mimi nimetumwa na Mungu,” alisema Cristo.
ANASWA NA KASHFA YA UTAPELI
Akiwa amejiamini na kujijengea heshima kubwa kwa waumini wake, Januari Mosi mwaka huu, mhubiri huyo alishambuliwa kwa maneno na watu wasiojulikana kwa kusambaza nyaraka za wazi zilizokuwa zimeandikwa kuwa yeye ni tapeli mkubwa kwani anadanganya watu ili kujipatia fedha.

Kitendo
hicho kilimpunguzia umaarufu kwani alikuwa ameweka utaratibu kwa
waumini wake kulipa fungu la kumi kwa kila pato, alijiweka zaidi kwa
wafanyabiashara wakubwa nchini Brazil huku akiwaonya kuwa bila yeye
hawawezi kufanikiwa kimaisha.
HISTORIA YAKE KIDUNIA
Cristo aliyezaliwa Machi 22, 1948 mwenye wafuasi wengi katika kanisa lake, amewahi kutembelea nchi nyingi duniani akieneza uzushi huo kwamba yeye ni Yesu Kristo.
Cristo aliyezaliwa Machi 22, 1948 mwenye wafuasi wengi katika kanisa lake, amewahi kutembelea nchi nyingi duniani akieneza uzushi huo kwamba yeye ni Yesu Kristo.
Amewahi
kufukuzwa kwenye baadhi ya nchi za Ulaya na Amerika ya Kusini zikiwemo
Uingereza, Venezuela, Peru, Marekani na Ufaransa ambako alitaka
kuanzisha makanisa. Pia ameshawahi kuwekwa ndani mara 40 nchini mwake
kutokana na kujitangaza kuwa yeye ni Yesu na kuvuta watu wengi.
Katika
nchi yake, Cristo amefanikiwa kuwafanya waumini wake waishi pamoja naye
kwenye makazi jirani na kanisa lake la Santa Catarina.
Wazazi wa mzee huyo, baba Wilhelm na mama Magdalena Thais ni Wakatoliki wenye asili ya nchini Ujerumani.
Tangu
mwaka 1979, Cristo amesafiri zaidi ya nchi 27 duniani kote akieneza
neno lake huku akisema yeye ni Mfalme wa Wayahudi aliyerejea duniani kwa
mara ya pili. Pia husema eneo la kanisa lake ni Yerusalemu mpya.
MAVAZI YAKE
Mara zote, Cristo huvaa kanzu nyeupe na viatu vya ‘makubazi’ huku kichwani akiwa na mduara wenye kuashiria taji la miiba alilovalishwa Yesu wa kweli.
Mara zote, Cristo huvaa kanzu nyeupe na viatu vya ‘makubazi’ huku kichwani akiwa na mduara wenye kuashiria taji la miiba alilovalishwa Yesu wa kweli.
ETI ALIISIKIA SAUTI YA MUNGU
Katika mahojiano yake na baadhi ya redio nchini humo, mhubiri huyo amekuwa akisema tangu utotoni mwake alikuwa akiifuata sauti ya Mungu ambayo ilikuwa ikisema: “Mimi ni Baba yako. Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.”

ANA MPANGO WA KUTEMBELEA AFRIKA
Inasemekana wakati wowote mwaka huu, Cristo atatembelea nchi mbalimbali za Bara la Afrika kwa lengo la kuvuta wafuasi wengi.
Inasemekana wakati wowote mwaka huu, Cristo atatembelea nchi mbalimbali za Bara la Afrika kwa lengo la kuvuta wafuasi wengi.
Nchi
za Zimbabwe, Afrika Kusini, Tanzania, Togo, Mali, Misri, Angola,
Nigeria, Burkina Faso na Zaire zinadaiwa kuwepo kwenye ratiba ya ‘Yesu’
huyo.
VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMKEMEA
Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wachungaji na maaskofu wa Tanzania kusikia wanamzungumziaje mhubiri huyo feki.
Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wachungaji na maaskofu wa Tanzania kusikia wanamzungumziaje mhubiri huyo feki.
MCHUNGAJI MTIKILA
Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation Church la jijini Dar es Salaam, Christopher Mtikila alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na sakata hilo, alisema:
Mchungaji wa Kanisa la Full Salvation Church la jijini Dar es Salaam, Christopher Mtikila alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusiana na sakata hilo, alisema:
“Huyo ni shetani mkubwa, akija Tanzania hatutaki kumwona kwani anakuja kuwavuruga waumini wetu.”
ZAKARIA KAKOBE
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lenye makao yake makuu kwenye Jiji la Dar es Salaam, Zakaria Kakobe naye alikuwa na haya ya kusema:
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lenye makao yake makuu kwenye Jiji la Dar es Salaam, Zakaria Kakobe naye alikuwa na haya ya kusema:
“Huyo akija Dar anatakiwa tumuombee ili mapepo yamtoke, awe mzima na amsifu Mungu.”
Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi nalo la jijini Dar, Lusekelo Antony ‘Mzee wa
Upako’ alisema utabiri wa Yesu kuwa nyakati za mwisho wengi watajitokeza
wakidai ni Kristo umetimia.
“Hizi
ni nyakati za mwisho kweli. Yesu alisema watatokea manabii wengi
wakisema wao ndiyo Kristo, ndiyo hao sasa. Hataweza kuushinda utawala wa
Mungu aliye hai,” alisema Mzee wa Upako.
CREDIT;HABARIZETUBLOG